Mkurugenzi  wa Kitengo  cha Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu cha Dodoma, Bi. Rose Joseph  leo Jumamosi tarehe 24 Mei 2025, katika Ukumbi wa LT2  (CHSS)  UDOM amefanya  Uzinduzi wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosomea Uandishi wa Habari na Uhusiano wa Umma Chuo Kikuu cha Dodoma - The University of  Dodoma Public Relations Students Association (UDOPRESA) yenye jumla ya wanachama 250. 

Taasisi hiyo imeanzishwa kwa dhamira kuu ya  kuwaunganisha wanafunzi wanaosoma Taaluma ya Uhusiano na Umma  na Uandishi wa Habari wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Kuimarisha Taaluma, Kushirikiana katika Tafiti na Mafunzo na kuwa chachu ya Maendeleo ya Taaluma hiyo Nchini. 

Akizungumza wakati wa Hafla ya  Uzinduzi;  Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu cha Dodoma Bi. Rose Joseph ameahidi kuwapa ushirikiano wowote watakaohitaji huku akiwaasa kutumia Taasisi hiyo katika kulinda taswira ya Chuo na  kuwataka watangulize uzalendo kwa Taifa mbele, kulinda na kuheshimu fani hiyo; pamoja na kuzingatia Sheria, Taratibu na Miongozo yote ya maafisa Uhusiano na Habari. 

"Hili ni Jukwaa muhimu sana ambalo si tu kwamba linawaleta pamoja wanafunzi wanaosomea Uhusiano wa Umma UDOM, lakini naamini ni jukwaa zuri la kuwanoa, kuwaweka tayari kwa ajili ya kwenda kulitumikia Taifa, kutetea Tasnia na  kwenda kuwa waandishi bora na maafisa bora wa umma" Aliongeza Bi. Rose. 

Kwa Upande wake; Mkuu wa Idara ya Sanaa na Taaluma za Habari, Dkt. Deograsia  Ndunguru amewapongeza Wanachama wote wa UDOPRESA huku akisisitiza kuwa Taasisi hiyo itawasaidia kuongeza ujuzi, Maarifa hasa katika kuwajenga kuwa maafisa Uhusiano Bora wa baadae. 

Naye; Mlezi wa Taasisi hiyo Dkt. Mary Kafyome,  amesema ulikuwa ni mchakato mkubwa kufanikisha jambo hilo huku akitoa pongezi kwa wote walihusika kufanikisha tukio hilo na ametoa wito kwa wanafunzi wanaobaki kuendeleza taasisi hiyo."UHUSIANO BORA, JAMII BORA!"

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko Chuo kikuu cha Dodoma Bi. Rose Joseph akikata keki kama ishara ya Uzinduzi wa Taasisi ya UDOPRESA  kutoka kulia kwake ni Mkuu wa Mkuu wa Idara ya Sanaa na Taaluma za Habari Dkt. Deograsia Ndunguru, akifuatiwa na Mlezi wa UDOPRESA Dkt. Mary Kafyome na Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa UDOPRESA Bw. Swerd Mwakage akifuatiwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Huduma za Wanafunzi UDOM Bw. Gabriel Elia.

Mgeni Rasmi Bi. Rose Joseph  akikabidhi Cheti cha Uongozi Bora kwa Mwenyekiti wa UDOPRESA Bw.Swerd Mwakage wakati wa Uzinduzi wa Taasisi hiyo

Mgeni Rasmi kwenye Hafla ya uzinduzi wa chama cha UDOPRESA, Bi. Rose Joseph akihutubia wakati wa uzinduzi

Mlezi wa Taasisi ya UDOPRESA  Dkt. Mary Kafyome akitoa neno la Shukurani wakati wa Uzinduzi wa Hafla ya UDOPRESA

Mkuu wa Idara ya Sanaa na Taaluma za Habari Chuo Kikuu cha Dodoma Dkt. Deograsia Ndunguru akitoa neno wakati kwa Washiriki wakati wa Uzinduzi wa Taasisi hiyo
Wanachama wa UDOPRESA wakiwa katika hali ya furaha wakati wa Uzinduzi wa Taasisi hiyo
Kamati ya Uzinduzi wa UDOPRESA ikikabidhi zawadi ya Picha kwa Mgeni Rasmi Bi. Rose Joseph katika Hafla ya Uzinduzi wa Taasisi hiyo

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...