Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na Agha Khan Foundation, Tanzania leo tarehe 20/05/2025 wamepanda miti zaidi ya 200 katika zoezi la kulinda mazingira kwa kuanzisha msitu bustani.

Zoezi hilo ni katika kuelekea Maadhimisho ya Miaka 50 ya TET yanayotarajia kufanyika Juni mwaka huu, limefanyika katika Makao Makuu ya TET, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba ameishukuru Agha Khan Foundation kwa hatua hiyo kwani wanatekeleza kwa vitendo utunzaji wa mazingira na kulinda mabadiliko ya tabianchi.

"TET katika kusheherekea Miaka 50 inaendeleza utunzaji wa mazingira kwa vitendo kwani hata katika maboresho ya mitaala ya kielimu tumezingatia utunzaji mazingira.

"Maboresho ya mitaala ya mwaka 2023 yameweka somo la jiografia kuwa ni somo la lazima na katika somo hilo tumewezesha wanafunzi kuhimili na kutunza mazingira," amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Programu wa Agha Khan Foundation Tanzania, Bi. Carolyn Mlewa amesema wamepanda miti hiyo zaidi ya 200 yenye aina 25 tofauti ikiwemo ya kivuli, matunda, dawa, na miti pori kama ishara ya kulinda mazingira.

"Hii ni katika kuendeleza ushirikiano wetu na TET katika uhimilivu wa tabianchi, ni mabadiliko ya tabia na namna ya kulinda hali hiyo, hivyo kupanda miti hiyo ambayo itakuwa na umuhimu mkubwa katika kulinda mazingira," amesema Bi. Mlewa.

Naye Msimamizi wa Mradi wa Mazingira wa taasisi hiyo, Japhet Wangwe amesema amesema upandaji msitu huo mdogo ni moja ya hatua ya kuboresha mazingira lakini pia kuhifadhi viumbe vya asili na vya Kiikolojia.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...