Na Seif Mangwangi,Arusha

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), imefanikiwa kudhibiti baa la panya katika mikoa 16 wilaya 54 na kata 540 na kuokoa jumla ya ekari Laki358,895 za mazao ikiwemo mahindi yaliyokuwa yaharibiwe na wadudu hao.

Aidha mamlaka hiyo imefanikiwa kudhibiti ndege aina kwelea kwelea zaidi ya milioni 80 katika Halmashari 24 nchini na kuokoa zaidi ya tani Milioni moja na laki moja (1100,000),za mazao mbalimbali zilizokuwa ziharibiwe ikiwemo mpunga uwele na mtama.

Hayo yameelezwa leo Mei 12, 2025 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya afya ya mimea na viatilifu Tanzania (TPHPA), Profesa Joseph Ndunguru kwenye maadhimisho ya siku ya afya ya mimea duniani ambapo kitaifa iliazimishwa jijini Arusha.

Akisoma taarifa ya mafanikio ya taasisi hiyo, Profesa Nduguru amesema pia katika kipindi cha mwaka mmoja TPHPA imefanikiwa kutokomeza viwavi jeshi waliokuwa wakitaka kuteketeza ekari 207.5 za mazao na hivyo kuokoa zaidi ya tani 500 za mazao ya nafaka ikiwemo mahindi katika mashamba mbalimbali nchini.

“ Mheshimiwa Mgeni rasmi, pia tumeweza kupambana na Nzige ambapo katika kipindi cha mwaka mmoja tulifanikiwa kuteketeza nzige waliovamia ekari 1340 katika wilaya ya mpwapwa mkoa wa Dodoma pamoja na nzige wekundu Milioni 36 waliovamia ekari 405 wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida,”amesema.

Amesema TPHPA ina mchango mkubwa katika utoshelevu wa chakula kwa asilimia 128 kutokana na jitihada zake za kudhibiti visumbufu vya mazao ambavyo vingeweza kuathiri uzalishaji wa mazao hayo.

Aidha amesema kupitia huduma za ukaguzi na udhibiti wa mazao mbalimbali mipakani TPHPA iliwezesha usafirishaji wa tani 5.5m za mazao mbalimbali ikiwemo mbogamboga, matunda, mikunde, viungo yenye thamani ya Dola za kimarekani bilioni 6.6 sawa na Tzs Trilion 15.6.

Amesema malengo ya baadae kuendelea kuimarisha udhibiti wa visibility kwa njia ya kibaiolojia viuatilifu hai, viumbe rafiki na kuwajengea uwezo wataalam katika kusimamia udhibiti wa visumbufu DNA.

Aidha profesa Ndunguru amesema wameshanunua ndege mpya maalum kwaajili ya kuulia nzige na kuondokana na usumbufu wa kuomba ndege kutoka shirika la nzige Kenya kwaajili ya kazi hiyo.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dkt. Stephen Nindi amesema Serikali itaendelea kuboresha mamlaka hiyo ili iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi wa hali ya juu na kuleta tija kwa Taifa.

Amesema usalama wa chakula ni miongoni mwa vipaumbele vikuu ndani ya Wizara ya kilimo hivyo afya ya mimea itaendelea kutiliwa mkazo ili kuleta tija kwa wakulima wengi zaidi nchini.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...