UPANDE wa Jamuhuri katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi katika kesi hiyo upo kwenye hatua za mwisho kukamilika.
Pia mahakama katika uamuzi wake mdogo imesema kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwa njia ya kawaida, ana kwa ana – tofauti na uamuzi wa awali uliokuwa unaruhusu kesi kusikilizwa kwa njia ya mtandao.
Aidha imewataka wanaoudhuria kesi kuacha mihemko ya kelele mahakamani.
Mapema wakili wa serikali Mkuu Nassoro Katuga alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franko Kiswaga kwamba kesi hiyo leo Mei 19, 2025 ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika
Kufuatia taarifa hiyo, Mawakili wa utetezi, Peter Kibatala na Rugemeleza Nshala walihoji kinachokwamisha upelelezi kutokamilika.
Wakili Katuga alidai kuwa upelelezi upo katika hatua za mwisho kukamilika, pia hawezi kueleza hadharani kitu kinachokwamisha upelelezi kutokamilika kwa wakati, labda wakipewa siku 14.
Baada ya kueleza hayo, Mawakili wa utetezi waliibua hoja za maombi madogo ya kwamba Mahakama itoe amri Askari Magereza wanaomlinda Lissu kizimbani watoke nje maana mteja wao bado ni mshtakiwa bado hajakutwa na hatia hadi pale mahakama itakaposema.
Pia mahakama itoe tamko la kuendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo kwa njia ya kawaida na sio kwa njia ya mtandao.
Katika uamuzi mdogo, Hakimu Kiswaga amesema kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwa njia ya kawaida, pia tarehe ijayo Mahakama ifanye uchunguzi juu ya usalama wa eneo ili kuwa na uhakika na usalama wa mtuhumiwa na hakuna tishio lolote la kiusalama basi mshtakiwa aachwe mwenyewe kizimbani.
Mbali na hilo, Hakimu Kiswaga amesema tarehe ijayo kila mtu ahakikishe hakuna kelele zozote za mihemko ya wanachama wa chama hicho na wahusika waendelee kuwaelekeza misingi ya mahakama.Kesi imeahirishwa hadi Juni 2, 2025.
Katika kesi hiyo inadaiwa Aprili 3, 2025 jijini Dar es Salaam mshtakiwa Lissu akiwa ndani ya jiji la Dar es Salaam alitangeneza nia ya kushawishi au kuchochea umma ya kuweza kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Tanzania kwa kusema maneno yafuatayo
"Walisema msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi tutahamasisha uasi, hiyo ndio namna ya kupata mabadiliko....kwa hiyo tunaenda kukinukisha sanasana huu uchaguzi tutaenda kuvuruga kwelikweli, tunaenda kukinukisha vibaya sana.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...