Joseph Masolwa Misalaba, Kaimu Katibu Mkuu na Mgombea wa Ukatibu Mkuu

Na. Mwandishi wetu,
CHAMA cha walimu Tanzania (CWT) kimetangaza kufanyika kwa mkutano mkuu wa chama hicho tarehe 28 na 29 mwezi mei mwaka huu mkutano ambao pamoja na mambo mengine utahusisha uchaguzi wa viongozi wa kitaifa

Taarifa kutoka ofisi ya katibu mkuu wa chama hicho mwalimu Joseph misalaba ambaye kwa sasa anakaimu nafasi hiyo imeeleza kuwa mkutano huo wa saba unafanyika baada ya chama hicho kukamilisha chaguzi za ngazi za chini ambazo ni ngazi ya shule, ngazi ya wilaya na mkoa ambapo hivi sasa wanaelekea kwenye ngazi ya Taifa.

Taarifa hiyo iliyosasainiwa na Afisa habari na mahusiano wa chama hicho inazitaja nafasi zinazotarajia kugombewa kuwa ni rais wa chama, makamu wa rais wa chama, katibu mkuu, naibu katibu mkuu na mweka hazina wa chama hicho

Nafasi nyingine ni mwakilishi wa walimu wanawake, mwakilishi walimu walemavu, mwakilishi walimu vijana na wadhamini wa chama.
Nashon Amos Kidudu, Kaimu Mweka Hazina na Mgombea wa nafasi hiyo tena

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...