Dar es Salaam, Mei 2, 2025 — Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, ameizindua rasmi Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL), huku akitoa wito kwa wajumbe wa bodi hiyo kufanya kazi kwa weledi, ufanisi na uwajibikaji ili kuliongezea shirika hilo tija na mchango chanya kwa taifa.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Prof. Mbarawa alisisitiza umuhimu wa kuboresha huduma kwa wateja na kuimarisha utendaji wa ndani kupitia mafunzo maalum kwa wafanyakazi wote.
“Ninaitaka bodi hii kuhakikisha inasimamia uboreshaji wa huduma kwa wateja, kuwepo kwa ratiba za kuaminika, bei za ushindani, matumizi ya teknolojia ya kisasa, pamoja na upanuzi wa mtandao wa safari,” alisema Prof. Mbarawa.
Waziri huyo pia alielekeza bodi kuweka mkazo katika kuingia mikataba ya ushirikiano na mashirika mengine ya ndege duniani, kuimarisha usimamizi wa rasilimali, na kuendesha kampeni madhubuti za masoko ili kuongeza ushindani wa kibiashara.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Air Tanzania, Bw. Peter Ulanga, alisema hadi sasa shirika hilo lina jumla ya ndege 16, ikiwa ni ishara ya uwekezaji mkubwa uliowekezwa na serikali katika sekta ya usafiri wa anga.
“Tunaishukuru serikali kwa kuendelea kuliwezesha shirika letu. Sasa jukumu letu ni kuhakikisha uwekezaji huu unaimarishwa kwa huduma bora na usimamizi makini,” alisema Bw. Ulanga.
Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo mpya, Profesa Neema Mori, aliahidi kuwa bodi yake itafanya kazi kwa uadilifu na weledi ili kuhakikisha Shirika la Air Tanzania linakuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa.
“Tutahakikisha tunatekeleza majukumu yetu kwa ufanisi na kwa kuzingatia maslahi mapana ya shirika na nchi kwa ujumla,” alisema Prof. Mori.
Uzinduzi wa bodi hiyo mpya unalenga kuleta msukumo mpya katika uendeshaji wa Shirika la Ndege la Taifa, huku matarajio yakiwa ni kuliona likijiimarisha kimataifa na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi wa taifa kupitia sekta ya usafiri wa anga.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...