Na Mwandishi Wetu
KADA wa CCM na mwanahabari Bakari Kimwanga amechukua fomu ya kuwania udiwani katika ya Makurumla ,Magomen mkoani Dar es Salaam ambapo anatetea tena nafasi hiyo ambayo ameitumikia kwa kipindi cha miaka mitano.
Kimwanga amechukua fomu hiyo na kuikabidhi leo Juni 29,mwaka 2025 kwa Katibu wa Kata wa CCM Makurumla, Omari Suleiman Bakari
Akizungumza baada ya kukabidhi fomu hiyo, Kimwanga ambaye pia ni mwanahabari alisema kuwa anajivunia kazi kubwa aliyoifanya kwa miaka mitano na sasa anaomba fursa kwenye kukamilisha maeneo yaliyobaki ili kujenga jamii yenye ustawi.
"Ninamaliza miaka mitano ya mafanikio ambapo sisi Makurumla tumefanikiwa kutekeleza miradi ya zaidi ya bilioni 18 ikiwamo barabara, kituo cha afya na elimu.
"Miaka mitano ijayo tunakwenda kujenga kata yenye kasi zaidi na muonekano mkubwa wa maendeleo kwa jamii, wana Makurumla na wana CCM ni watu wema sana nyakati zote tumekuwa pamoja na Mungu akipenda ikiwa chama itawapendeza jina likarudi kwenye uteuzi sina shaka na maamuzi yao kwangu na chama chetu ni ushindi," amesema Kimwanga

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...