Kassim Nyaki, NCAA Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amewavisha cheo manaibu kamishna wawili na kushuhudia uvishwaji vyeo kwa makamishna wasaidizi waandamizi watano waliovishwa vyeo na mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi NCAA Jenerali Venance Mabeyo (Mstaafu)

Waliovishwa Cheo na Mhe. Waziri ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Joas John Makwati aliyepandishwa cheo kuwa Naibu Kamishna wa Uhifadhi anayesimamia Uhifadhi, utalii na Maendeleo ya Jamii na Naibu Kamishna wa Uhifadhi Aidan Paul Makalla anayesimamia Huduma za Shirika NCAA.

Kwa upande wa makamishna waliovishwa vyeo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NCAA Jenerali Venance Mabeyo (mstaafu) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia idara ya Mipango na uwekezaji, Gasper Stanley Lyimo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Paul Geofrey Shaidi anayesimamia Kitengo cha huduma za Sheria, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Charles Marwa Wangwe anayesimamia Idara ya Uhasibu na fedha.

Wengine ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Godwin Felician Kashaga anayesimamia Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, na Afisa Uhifadhi Mkuu Daraja la kwanza Mariam Kobelo anayesimamia idara ya Huduma za Utalii na masoko aliyepandishwa cheo kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi.

Baada ya kuwavishwa vyeo hivyo waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amewaelekeza maafisa hao kufanya kazi kwa bidiii na weledi mkubwa katika kutekeleza majukumu yao kwa kuwa cheo ni dhamana na kinakuja na majukumu.

“Nimatumaini yangu kuwa viongozi wote mliovaa vyeo leo mtakuwa chachu ya kufanya kazi kwa kujituma na kuonesha mfano wa kuigwa kwa Maafisa na Askari mnaowaongoza, juhudi zenu ndiyo zitakazochangia kulinda na kuhifadhi eneo la Ngorongoro na kuendelea kuwa kivutio kwa wageni wanaotembelea” ameongeza Balozi Chana.

Kamishna wa Uhifadhi NCAA Abdul-Razak Badru ameeleza kuwa kwa sasa watumishi wote wa NCAA wameshapatiwa mafunzo ya kijeshi kutoka mfumo wa awali wa kiraia na kuwa mamlaka hiyo itahakikisha inatumia rasilimali ya watumishi waliopo kuongeza nguvu ya kuhifadhi, kulinda, kuendeleza jamii na kuboresha miundombinu ya utalii.

Mwenyekiti wa bodi ya NCAA Jenerali, Venance Mabeyo (mstaafu) ameeleza kuwa mafanikio ya Ngorongoro yanategemea uadilifu na uwezo wa viongozi wake na kuwaasa viongozi waliovishwa vyeo kubeba matumaini mapya katika utekelezaji wa majukumu ya uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii.

Mabeyo amempongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Serikali kwa ujumla na wadau wa utalii kwa kuiunga mkono Ngorongoro na hatimae kutangazwa kama Kivutio Bora cha Utalii Barani Afrika kwa mwaka 2025.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...