Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz Tanzania, wameendesha semina maalum kwa wakandarasi wa Zanzibar wakilenga kuwajengea uwezo zaidi wakandarasi hao ili waweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo visiwani humo kwa ufanisi zaidi kupitia huduma bora za kifedha na bima zilizobuniwa mahususi kwa ajili yao.

Warsha hiyo iliyofanyika jana Zanzibar iliongozwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed ilihusisha uwepo wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Habiba Hassan Omar, wakandarasi, maofisa wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa Madeni na Masoko ya Mitaji wa benki hiyo, Bw Zubeir Masabo pamoja na maofisa wa kampuni ya Jubilee Insurance wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Uhakiki Bw Yassin Ally Masenza.

Akizungumzia hatua hiyo, Dkt Khalid pamoja na kuzipongeza taasisi hizo warsha hiyo muhimu, alisema hatua hiyo kwa kiasi kikubwa itaisaidia serikali kufanikisha kwa urahisi dhamira yake ya msingi ya ujenzi wa miundombinu visiwani humo, kwa kuwa miradi mingi inatekelezwa na wakandarasi wazalendo ambao baadhi yao bado wanakabiliwa na changamoto ya rasilimali fedha na ukosefu wa huduma sahihi za bima kwenye miradi yao.

“Zanzibar kwa sasa imeweka vipaumbele vikuu vinne; miundombinu ya usafiri na uchukuzi, uchumi wa buluu, huduma za kijamii kama elimu, afya, maji safi na salama, umeme pamoja na utalii. Utekelezaji wa miradi yote inayogusa maeneo haya unahitaji rasilimali fedha ya uhakika pamoja na kinga yanapotokea majanga ya asili kama mafuriko, moto na vimbunga. Jitihada hizi za wadau hawa wawili zitasaidia kuwajengea uelewa na kufungua fursa kwa wakandarasi wetu ili wawe na majibu sahihi katika kufanikisha miradi hii kwa wakati na kwa ufanisi zaidi,’’ alisema Dkt Khalid.

Zaidi, Dkt Khalid alielezea kuridhishwa kwake na ushirikiano unaoendelea baina ya serikali na mashirika na taasisi binafsi katika kufanikisha miradi mbalimbali kwa maendeleo ya taifa.

“Hivyo ni matumaini yetu kuwa baada ya semina hii wakandarasi wetu hususani wazalendo watanufaika na elimu hii, na wataitumia kama chachu katika kufanikisha utekelezaji wa miradi kwa viwango vya juu zaidi. Serikali kama mdau wao mkubwa zaidi tunahitaji kuona miradi yetu inatekelezwa kwa ubora unaozingatia thamani ya fedha na muda,” aliongeza Dkt. Khalid.

Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, Bw Masabo alisema benki hiyo imejipanga kutoa huduma mahsusi kwa ajili ya kuwawezesha wakandarasi wa ndani kupata fedha na usaidizi wa kifedha kwa urahisi, kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundobinu kwa wakati na ubora uliokusudiwa.

“NBC tunatambua kuwa maendeleo ya sekta ya ujenzi ni kichocheo kikuu cha maendeleo ya taifa. Na hili kufanikisha hili ni lazima wakandarasi wetu hususani wazalendo wawe na uwezo mkubwa kifedha ili waweze kushindana na wenzao kutoka nje ya nchi. Pamoja na mafunzo haya kuhusu huduma zetu mahususi kwao, tumejipanga zaidi kwenye kutoa huduma bora na rafiki kwa wakandarasi ili waweze kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo,” alisema Masabo.

Bw Masabo alitaja baadhi ya huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa wakandarasi kuwa ni pamoja na dhamana na mitaji (Working capital guarantee facilities) kwa ajili ya kuombea zabuni mbalimbali, mikopo ya muda mrefu ya zaidi ya miaka mitano hadi saba, Uhandisi na Ununuzi pamoja na Ufadhili (EPC +F), na kutoa mikopo kwenye miradi ya ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Uhakiki wa Bima kutoka Jubilee Allianz Tanzania, Bw Yassin Ali Masinza alisema kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na benki ya NBC na wakandarasi kwa kutoa huduma za bima zinazowalinda dhidi ya hatari na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi yao mbalimbali

“Tumejifunza kuwa changamoto kubwa kwa wakandarasi ni upatikanaji wa huduma za bima kwa wakati na kwa gharama nafuu. Jubilee Insurance tupo tayari kuandaa bidhaa maalum zinazolenga mazingira ya wakandarasi wa Zanzibar,” alisema Bw Masinza.

Warsha hiyo ilihitimishwa kwa mijadala ya wazi ambapo wakandarasi walipata fursa ya kuuliza maswali, kubadilishana uzoefu na kupata mrejesho kutoka kwa wataalamu wa NBC, Jubilee Insurance na taasisi nyingine washirika.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed (katikati) akijadili jambo na Mkuu wa Madeni na Masoko ya Mitaji wa benki ya NBC Bw Zubeir Masabo wakati alipowasili ili kuzindua rasmi  semina maalum kwa wakandarasi wa Zanzibar iliyoandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz Tanzania ikilenga kuwajengea uwezo zaidi wakandarasi hao ili waweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo visiwani humo kwa ufanisi zaidi kupitia huduma  bora za kifedha na bima zilizobuniwa mahususi kwa ajili yao. Semina hiyo ilifanyika jana Zanzibar. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Habiba Hassan Omar na Mkuu wa Idara ya  Sekta ya Umma wa Benki ya NBC  Bi Joyce Maruba (wa pili kushoto)

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed (kushoto) akizungumza na wakandarasi waliohudhuria semina maalum iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz Tanzania ikilenga kuwajengea uwezo zaidi wakandarasi hao ili waweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo visiwani humo kwa ufanisi zaidi kupitia huduma  bora za kifedha na bima zilizobuniwa mahususi kwa ajili yao. Semina hiyo ilifanyika jana Zanzibar.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed (kushoto) akijadili jambo na Mkuu wa Madeni na Masoko ya Mitaji wa benki ya NBC Bw Zubeir Masabo (kulia) wakati wa semina maalum kwa wakandarasi wa Zanzibar iliyoandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz Tanzania ikilenga kuwajengea uwezo zaidi wakandarasi hao ili waweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo visiwani humo kwa ufanisi zaidi kupitia huduma  bora za kifedha na bima zilizobuniwa mahususi kwa ajili yao. Semina hiyo ilifanyika jana Zanzibar.

Mkuu wa Madeni na Masoko ya Mitaji wa benki ya NBC Bw Zubeir Masabo (katikati) akizungumza na washiriki wa semina maalum iliyoandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz Tanzania ikilenga kuwajengea uwezo zaidi wakandarasi visiwani Zanzibar ili waweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo visiwani humo kwa ufanisi zaidi kupitia huduma  bora za kifedha na bima zilizobuniwa mahususi kwa ajili yao. Semina hiyo ilifanyika jana Zanzibar.

Mkuu wa Madeni na Masoko ya Mitaji wa benki ya NBC Bw Zubeir Masabo (kushoto) na Mkuu wa Idara ya  Sekta ya Umma wa Benki ya NBC  Bi Joyce Maruba (katikati) wakijadili jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Zanzibar,  Dkt Habiba Hassan Omar, wakati wa semina maalum iliyoandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz Tanzania ikilenga kuwajengea uwezo zaidi wakandarasi visiwani Zanzibar ili waweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo visiwani humo kwa ufanisi zaidi kupitia huduma  bora za kifedha na bima zilizobuniwa mahususi kwa ajili yao. Semina hiyo ilifanyika jana Zanzibar.




Semina hiyo ilihusisha mijadala ya wazi ambapo wakandarasi walipata fursa ya kuuliza maswali, kubadilishana uzoefu na kupata mrejesho kutoka kwa wataalamu wa NBC, Jubilee Insurance na taasisi nyingine washirika.


Maofisa wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa Madeni na Masoko ya Mitaji wa benki ya hiyo Bw Zubeir Masabo (Katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa semina hiyo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...