Na Pamela Mollel Arusha,
Katika sekta ya utalii nchini Tanzania, jina la Chacha Nyandongo si geni tena. Akiwa na zaidi ya miaka 20 ya uzoefu kama mwongoza watalii, Chacha amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na weledi, uzalendo na mapenzi yake katika kazi ya kuongoza watalii nchini Tanzania
Kwa sasa, Chacha anawakilisha kampuni ya Ndoto Kubwa Tours, yenye makao yake makuu jijini Arusha. Kupitia kampuni hiyo, amewahudumia watalii kutoka mataifa mbalimbali duniani, akieleza kwa umahiri uzuri wa mbuga za wanyama, milima, maziwa, na tamaduni za makabila mbalimbali ya Tanzania.
Licha ya mafanikio hayo, Chacha haachi kuonesha upande wa pili wa kazi hii,anaeleza changamoto kubwa zinazoikumba sekta ya waongoza watalii. Anasema kuwa wengi wao hukumbwa na mishahara midogo na hukosa huduma muhimu kama bima ya afya, jambo ambalo huwalazimu wakati mwingine "kujishusha kwa mgeni ili apate chochote," ili kuweza kujikimu.
"Tunajitahidi kufanya kazi kwa bidii, lakini bado mazingira si rafiki. Tunaiomba serikali kupitia Wizara iingilie kati na kuweka sera zitakazoboresha maslahi ya waongoza watalii hapa nchini" anasema Chacha kwa msisitizo.
Akiamini kuwa utalii ni uti wa mgongo wa uchumi wa taifa, Chacha anaamini kuwa mwongoza watalii bora ni yule anayependa nchi yake kwa dhati, na pia mwenye elimu ya kutosha ili aweze kuieleza Tanzania kwa ufasaha na uelewa kwa wageni.
"Tanzania tumejaliwa sana – tuna mbuga nzuri, Mlima Kilimanjaro, Serengeti, Ngorongoro, watu wakarimu… lakini haya yote hayawezi kuonekana kwa macho ya mgeni bila mwongoza watalii anayejua thamani yake," anasisitiza.
Aidha, Chacha anasisitiza kuwa waongoza watalii ni nguzo kuu katika mafanikio ya sekta ya utalii, kwa kuwa wao ndio hukaa na wageni muda wote wa safari – kuanzia uwanja wa ndege hadi mbugani, na hata wakati wa kuagana. Ni wao wanaobeba taswira ya taifa, wanaojibu maswali, kutafsiri tamaduni, na kuhakikisha usalama, faraja na furaha ya wageni.
“Mgeni hawezi kuifahamu Tanzania kupitia hoteli au vipeperushi. Anaifahamu kupitia mwongoza watalii wa kila siku. Hivyo basi, sisi ni mabalozi wa taifa kwa vitendo,” anasema Chacha.
Chacha Nyandongo ni mfano bora wa vijana wachapa kazi waliodhamiria kuibeba sekta ya utalii kwa moyo mmoja, akitoa wito kwa vijana wengine kuichukulia kazi hii kama wito wa kulitangaza taifa, si tu ajira ya muda mfupi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...