Farida Mangube, Kilombero, Morogoro.

Mkuu wa wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya, ameeleza mpango wa kuifanya wilaya hiyo kuwa eneo la mfano kitaifa katika kuendeleza vipaji pamoja na uwezo binafsi wa watoto na vijana, akisisitiza kupitia halmashauri zake mbili za Mlimba na Halmashauri ya Mji Ifakara, watasimamia utekelezaji wa mipango thabiti ya kuimarisha stadi za maisha kuendana na maboresho ya kwenye mitaala ya kufundishia.

Amebainisha hayo alipokuwa mgeni rasmi kwenye kufunga kambi ya wiki moja ya "Usiku wa Vipaji" iliyowakutanisha watoto na vijana kutoka vituo vya huduma ya Mtoto na Kijana vinavyosimamiwa na Umoja wa Makanisa wa Klasta ya Ifakara, kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la Compassion. 

Kambi hiyo ililenga kuwajengea uwezo washiriki katika kujieleza, kujitambua, a kutumia vipaji vyao kama msingi wa kujitegemea.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Klasta hiyo, Jovin Ngenzi, kambi hiyo ilikuwa ya aina yake, ikilenga kuweka misingi ya maendeleo ya watoto kupitia vipaji. Alisema lengo ni kuwaandaa watoto walio katika vituo hivyo kuwa na maarifa ya maisha ya kila siku, kwa kutumia vipaji kama nyenzo ya kujikwamua kiuchumi na kijamii.

Walezi na viongozi wa makanisa walioshiriki, akiwemo Askofu.Laurent Elius na Mchungaji Anthon Mwaego wa Kanisa la TAG Katindiuka, walieleza kuwa changamoto kubwa inayokwamisha mafanikio ya vijana ni kukosekana kwa mfumo rasmi wa kutambua na kufuatilia maendeleo ya vipaji vya watoto tangu shule za msingi. Walisema ipo haja ya ushirikiano wa karibu kati ya halmashauri, taasisi za kidini na jamii katika kukuza vipaji hivyo.

Zaidi ya watoto na vijana 200 kutoka vituo 12 vya Klasta ya Ifakara walishiriki, ambapo walionyesha vipaji mbalimbali vikiwemo Kuimbaji, uchoraji na michezo ya kuigiza. Kilele cha kambi hiyo kilitawaliwa na maonesho ya vipaji na washindi kutambuliwa kwa zawadi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...