Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Olivanus Thomas ametoa wito kwa wananchi wote Wilayani Ludewa mkoani Njombe kujiunga na vilabu vya mazoezi (Jogging Clubs) na kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili waweze kuimarisha afya zao na ustawi wa jamii.

Mkuu huyo wa wilaya alitoa wito huo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo yaliadhimishwa kwa shughuli ya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya mji wa Ludewa ambapo alitumia fursa hiyo kuwajulisha wananchi juu ya uzinduzi wa vikundi vya mazoezi utakaofanyika Juni 7 mwaka huu.

Sambamba na hilo amegawa sare za mazoezi kwa vikundi mbalimbali ambazo watazitumia wakati wa mazoezi hivyo amewataka wananchi kujiunga na vikundi hivyo kwani havipo kwaajili ya watu maalum bali kwaajili ya wananchi wote.

“Mazoezi ni muhimu kwa afya zetu. Jogging Club si tu kwamba itasaidia kuimarisha miili yetu, bali pia itatusaidia kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.”

























Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...