Na Mary Margwe, Simanjiro
Diwani wa Kata ya Endiamtu wilayani Simanjiro Mkoani Manyara amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa namna ambavyo amepeleka fedha zaidi ya bil. 10.5 Kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika kata hiyo.
Hayo amebainisha jana wakati akizungumza na Wananchi wa Kata hiyo Jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kitongoji cha Endiamtu, akielezea Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kipindi cha miaka mitano (2020-2025) ambapo ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha zaidi ya sh.bil.10.5 Kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Kata hiyo
Chimba amesema Sasa wakati umefika wa wananchi kuona jitihada mbalimbali zilizofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa namna alivyo peleka fedha nyingi za miradi mbalimbali ya Maendeleo katika kata, na hivyo amemshukuru kwa kuwapatia fedha za miradi mingi.
" Kuna ujenzi unaendelea katika Kata yetu ya Endiamtu Jengo la kitega uchumi la Tanzanite city ( soko la Madini ya Tanzanite) haya yote ni maono ya Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupenda na kutujali sisi wananchi wake ameona ni vema kutuwezesha Mradi huu kubwa na WA wenye zaidi ya gharama ya sh.bil.5.4, katuletea Mradi wa Maji katika Kata yetu wa zaidi ya bil.4.3, afya sh.mil.300.6 na miradi mingine katika sekta ya elimu Msingi na Sekondari kwa zaidi ya mil.500.
Amesema kama Diwani wa CCM amesimama katika Imani aliyoaminiwa na wananchi waliomweka madarakani, kwani wananchi wamemuamini na kumpa ridhaa ya kuwa Diwani wa Kata hiyo katika kipindi hiko Cha miaka mitano, na hivyo alichoahidi ametekeleza na vimeonekana.
" Kama mnavyofahamu Mimi sio mtu wa maneno nadhani mbanifahamu, na masuala ya Uongozi kwangu siwezi kabisa, siwezi kuahidi kitu nisichokiweza, nikisema nyeupe ujue ni nyeupe sio blue, huu sio wakati wa kuwadanganya wananchi waliokupa heshima kubwa na wakaniweka madarakani alafu, lazima niwatumikie kwa moyo wangu wote, iwe jua, iwe mvua niko nanyi, na ndio maana hata Sasa mvua imetunyeshea wote hakuna aliyeondoka, tumekubali wote tunyeshewe na mvua, nawashukuru sana kwa kuniamini kwenu" amesema Diwani wa Kata ya Endiamtu Lucas Zacharia Chimba.
Aidha WANANCHI wa Kata Endiamtu wilayani Simanjiro Mkoani Manyara nao wamempongeza Diwani wa Kata hiyo Lucas Zacharia Chimba kwa uwajibikaji wake wa utekelezaji wa Ilani ya CCM kikamilifu.
Wamesema Diwani huyo amekua ni kiongozi imara na mchapa kazi kweli kweli ukilingamisha na Diwani aliyekuwepo awali, Diwani Lucas Zacharia Chimba ndio hitaji la Wana Endiamtu kwa kile walichodai kuwa ni mkweli daima asiyependa kuwadanganya wananchi wake, ni mfuatiliaji na mjenga hoja za Msingi zenye kuwaletea wananchi mafanikio makubwa ndani ya Kata husika.
Akizungumza kwenye Mkutano huo mbele ya Diwani huyo Aponary Alex Massawe amesema tangu kuchaguliwa Kwa Diwani Lucas Zacharia Chimba kuwa Diwani wa Kata ya Endiamtu Maendeleo mbalimbali yameweza kupatikana ukilingamisha na kipindi kilichopita.
" Tangu kuchaguliwa kwako umefanya kazi KUBWA na nzuri katika jamii, umekua ni kiongozi mtiifu kwetu unayejua mipaka yako ya kazi na umuhimu wetu kama tuliokuweka madarakani , na hata siku zote umekua ukituita sisi mabosi wako, jambo ambalo Kwa wengine wangelenda kusikia masikioni kwao wakiitwa wao ndio mabosi, hakika hatukufanya makosa kukuchagua, na ,uda utafika utaongea tu, hatutababaika na wapita njia sisi" amesema Massawe.
Aidha amesema wanafahamu utendaji wake wa kazi, akua ni kiungo mkubwa katika kuwajenga na kuwaunganisha wananchi pamoja, Maendeleo yaliyofanyika ni mengi na makubwa sana.
" Tumesikia hapo Mtendaji wetu wa Kata bwana Charles Msangya amesoma taarifa kuwa Diwani wetu Mhe.Lucas Zacharia Chimba amekua ni mtu wa kujitolea katika kufanikisha miradi mbalimbali ya Maendeleo mfano umetengeneza madawati yapatayo 87 yenye thamani ya sh.mil.6,960,000 na changamoto ukaifutilia mbali kabisa hakika tunajivunia kuwa na wewe Diwani wetu,mumekua uliojitolea pesa zako za mfukoni ili kufanikisha jambo liende na sio kusimamia" ameongeza Massawe
Naye Salama Rajabu amesema taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM imesheheni mafanikio makubwa mfano ujenzi unaoendelea wa Jengo la soko la Madini ( Tanzanite city ) liko ndani ya Kata ya Endiamtu, Mradi ambao utakapokamilika wananchi wataweza kubadilisha maisha yao kupitia uwekezaji wake katika kufanya biashara mbalimbali za ujasiliamali na kujiongezea kipato.
" Hili jengo litakapokamilika hakika na maisha yetu nayo yatakua yamebadilika, kwani kila mmoja atakua akipambana na kujishughulisha na Biashara itakayoweza kutuingizia kipato na maisha yetu yakaenda mbele, Diwani wetu hongera sana umefanya makubwa katika Kata yetu, Ilani tumeisikia na hakika umeitekeleza vema, si vitu vya kupapasa ni vitu vyakuonekana laivu" amesema Salma Rajabu
Naye Mwenyekiti wa Tawi la Kazamoyo Fatuma kifunta amesema Ilani ya CCM imetekelezwa Kwa viwango vya juu kabisa , huku akisema Lucas Zacharia Chimba kuwa ni Diwani wa viwango.
" Hakika utekelezaji wa Ilani yetu ya CCM tumeisikia, miradi tumeisikia, hakika wewe ni Diwani wa viwango, umekua ukituita pesa ya familia yako Kwa ajili ya kutusaidia sisi wananchi ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa, ni nani ameweza kutoa pesa za mfukoni mwako sh. Mil.7 kasoro Kwa ajili ya kutatua changamoto ndani ya jamii, lakini wewe baba yetu, kaka yetu, mdogo wetu na kiongozi wetu umeweza, Mwenyezi Mungu aendelee kukusimamia na kukutetea wakati wote tuko na wewe" amesema kifunta.
Hata hivyo akipokea pongezi mbalimbali kutoka kwa wananchi hao Diwani wa Kata hiyo Lucas Zacharia Chimba amesema amepokea pongezi hizo Kwa mikono miwili, isipokua huku akisema kuwa wakushukuriwa ni Mungu na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye alepeleka fedha zaidi ya sh.bil.10.5 Kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika kata hiyo.

UTEKELEZAJI WA ILANI :Diwani wa Kata ya Endiamtu wilayani Simanjiro Mkoani Manyara Lucas Zacharia Chimba akizungumza na Wananchi wa Kata hiyo Jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kitongoji cha Kazamoyo, akielezea Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kipindi cha miaka mitano (2020-2025) ambapo ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha zaidi ya sh.bil.10.5 Kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Kata hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...