Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba amesema moja ya sababu zinazosababisha Watanzania wengi kuingia kwenye mikopo umiza pamoja na kausha damu ni kutokuwa na tabia ya kukopa fedha katika mifumo iliyo rasmi.

Dkt Nchemba ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa huduna za fedha zinazotolewa na taasisi zinazosimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania BoT(SEMA na BOT) pamoja na uzinduzi wa Mazingira ya majaribio ya teknolojia ya huduma za fedha yanayodhibitiwa na benki hiyo.

"Mtu anatafuta shilingi milioni moja ameshidwa kupata lakini anakwenda sehemu kukopa milioni moja anaambiwa arejeshe baada ya mwezi mmoja shilingi milioni tatu, sasa kama moja imemshinda hiyo tatu ataweza kweli.

“Hii yote ni kutokana na watu kuacha kukopa kwenye mifumo rasmi na kwenda kwenye hiyo kausha damu, kama mtu ungekwenda Benki hiyo milioni moja labada ungeambiwa hata urejeshe kwa mwaka mmoja au mitatu lakini kutokana na kuacha kuitumia mifumo rasmi matokeo yake ndiyo haya,”amesema

Amesema pia wapo watu ambao wanakopa fedha kwa kuweka dhamana ya shamba lenye mazao hali amabyo inawalazimu kuwa vibarua kwenye mashamba yao wenyewe.

“Unakopa fedha na kumwambia mtu utakuja kuchukua mahindi kiasi fulani kwa uwiano ambao siyo sawa kwako na kuendelea kuwa kibarua kwenye shamba lako mwenyewe sasa hii inatofauti gani na mababu zetu wakati wa ukoloni,”alisema Dkt. Nchemba

Aidha, Dkt. Nchemba ametoa maagizo kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kusimamia taasisi zote za fedha nchini kujiunga na mifumo ya malalamiko ya masuala ya fedha ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazojitikeza kwa watumiaji.

Naye Gavana wa Benki Kuu Tanzania Emmanuel Tutuba, amesema kutokana na uongozi na ushirikiano mzuri, uchumi ulikua kwa asilimia 5.5 mwaka 2024, ikilinganishwa na asilimia mfumuko wa bei ulikuwa wa wastani wa asilimia 3.1, na mikopo kwa sekta binafsi ilikua kwa wastani wa asilimia 12.7.

“Sekta ya fedha iliendelea kuwa imara na thabiti, yenye mtaji na ukwasi wa kutosha, yenye kutengeneza faida, na ubora wa rasilimali za mabenki uliendelea kuwa wa imara, ambapo uwiano wa mikopo chechefu ulikuwa asilimia 3.6 mwezi Februari 2025, ndani ya kiwango kinachokubalika cha chini ya asilimia 5.

Amesema, katika kukabiliana na changamoto zilizotajwa, Benki Kuu ya Tanzania, kupitia Baraza la Taifa la Huduma Jumuishi za Fedha, ilichukua hatua mbalimbali.

“Mojawapo ya matunda ya hatua zilizochukuliwa ni uzinduzi ambao utaufanya leo Mheshimiwa Waziri. Ninayo furaha kubwa kusimama mbele yako na mbele ya wadau wote waliopo hapa kuomba uzinduzi wa mambo haya mawili makubwa yanayolenga kuboresha mfumo wa utoaji wa huduma za fedha, yaani Mazingira ya majaribio ya Teknolojia ya Fedha ya Benki ya Tanzania (Bank of Tanzania Fintech Regulatory Sandbox) pamoja na Mfumo wa Kushughulikia Malalamiko ya Watumiaji wa Huduma za Fedha ujulikanao kwa jina la SEMA na BOT.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...