Juni 19, 2025 – Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida, leo amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi hiyo lililopo Mtaa wa Ardhi, Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Katika ukaguzi huo, Dkt. Kida amemwelekeza mkandarasi anayejenga mradi huo, Suma JKT, kukamilisha ujenzi na kukabidhi jengo hilo mapema iwezekanavyo kwa kuwa serikali imekamilisha sehemu kubwa ya malipo anayostahili mkandarasi huyo,
Aidha, alikumbusha mhandisi mshauri, ambaye ni Chuo Kikuu cha Ardhi, kuhakikisha anasimamia ubora ili jengo hilo liwe na hadhi na viwango vya juu vinavyoendana na thamani halisi ya fedha za Serikali.
Kwa sasa, mradi wa ujenzi wa jengo hilo upo katika hatua za mwisho ambapo imeelezwa kuwa umefikia asilimia 77. Jengo linatarajiwa kukabidhiwa rasmi Septemba, mwaka huu

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...