Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) limeingia kwenye ushirikiano rasmi na Tanzania Startup Association (TSA) kwa kusaini makubaliano ya ushirikiano (MoU) yenye lengo la kuziwezesha biashara changa (startups) kufikia masoko ya mitaji na kukuza mazingira ya ubunifu nchini.

Makubaliano hayo yamesainiwa katika hafla iliyofanyika katika ofisi za DSE jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi kutoka taasisi zote mbili, wawakilishi wa vyombo vya habari pamoja na wadau wa sekta ya mitaji na ubunifu.

Akizungumza katika tukio hilo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Startup Association, Ndg. Zahoro Muhaji, amesema ushirikiano huo ni hatua muhimu kwa ekosistimu ya ubunifu nchini, hususan kwa vijana wenye mawazo ya kibunifu lakini wanakosa maarifa au mitaji ya kuendeleza biashara zao.

“Makubaliano haya ni daraja la kuwaunganisha wabunifu wetu na fursa rasmi za masoko ya mitaji. Ni mwanzo wa safari ya mabadiliko ya kweli katika maendeleo ya biashara changa Tanzania,” alisema Muhaji.

Kwa upande wake, uongozi wa DSE umesisitiza kuwa ushirikiano huo unalenga kuvunja dhana kwamba masoko ya mitaji ni kwa makampuni makubwa pekee.

“Kupitia makubaliano haya, tunapanua wigo wa ushiriki wa vijana, wabunifu na wafanyabiashara wadogo kwenye soko la mitaji. Tunajenga mazingira jumuishi na endelevu ya uwekezaji,” ilieleza DSE.

“Makubaliano haya yanafungua ukurasa mpya kwa kizazi cha sasa na kijacho cha wafanyabiashara wa Kitanzania,” alisema Ndg. Zahoro Muhaji, Afisa Mtendaji Mkuu wa TSA, wakati wa hafla ya utiaji saini.

Kwa pamoja, DSE na TSA wamejipanga kuhakikisha mazingira wezeshi yanajengwa kwa ajili ya kuendeleza biashara zinazochipukia, kuongeza ujuzi wa kifedha na kuhimiza ushiriki wa sekta binafsi katika maendeleo ya taifa.







Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...