Dar es Salaam, Juni 16, 2025 — Kampuni ya Multichoice Tanzania, kupitia huduma yake ya DStv, imethibitisha dhamira yake ya kuendelea kuwa karibu na wateja wake kwa kuzindua kampeni mpya inayojulikana kama "Onja Utamu wa Mitanange", ikilenga kuwawezesha wateja kushuhudia michuano mikubwa ya FIFA kwa bei nafuu.
Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Masoko wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo, amesema kampeni hiyo inalenga kutoa fursa kwa kila Mtanzania, hasa wapenzi wa michezo, kupata uhondo wa michuano hiyo mikubwa duniani LIVE, kupitia kifurushi cha bei ya chini kabisa cha POA.
“Tunatambua umuhimu wa burudani ya michezo kwa wateja wetu. Kupitia kampeni ya 'Onja Utamu', sasa mteja yeyote akilipia kuanzia kifurushi cha POA, atapata nafasi ya kujionea mechi zote za michuano ya FIFA moja kwa moja, bila kulazimika kubadilisha kifurushi,” amesema Shelukindo.
Ameongeza kuwa lengo kuu ni kuhakikisha hakuna Mtanzania anayekosa kushuhudia burudani hiyo ya kipekee, huku akisisitiza kuwa Multichoice Tanzania itaendelea kuwekeza katika kuhakikisha huduma bora na zenye thamani kwa wateja wake zinapatikana kwa kila mtu — bila kujali uwezo wa kifedha.
Kampeni ya “Onja Utamu wa Mitanange” inakuja wakati ambapo mashabiki wa soka duniani kote wakiwa na hamasa kubwa kuelekea michuano hiyo mikubwa ya FIFA, na hivyo kuwa fursa adhimu kwa familia, marafiki na majirani kukusanyika pamoja na kufurahia burudani kupitia DStv.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...