Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) imesaini hati ya makubaliano ya kutoa mtaji wa jumla ya shilingi bilioni 63.2 kwa ajili ya kuziwezesha taasisi tatu za kifedha nchini Tanzania, ili kuongeza kasi ya utoaji mikopo kwa sekta muhimu zinazochochea maendeleo ya haraka ya kiuchumi.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo jijini Dar es Salaam, ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa EADB, Bernard Mono, amesema kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika sekta za nishati, viwanda, miundombinu na madini — sekta ambazo zina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Kamishna wa Uendelezaji Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya EADB, Charles Mwamaja, amesema kuwa lengo la uwezeshaji huo ni kuchochea mabadiliko ya haraka ya kiuchumi, kuongeza ujumuishaji wa kifedha na kuweka mazingira wezeshi kwa Watanzania wengi kunufaika na huduma za kifedha.
 
Taasisi zilizonufaika na mpango huo ni pamoja na Benki ya Maendeleo ya TIB ambayo imewezeshwa kwa mtaji wa shilingi bilioni 30, Azania Bank iliyopewa shilingi bilioni 13.3, na Taasisi ya Mikopo ya Nyumba (TMRC) ambayo imepata shilingi bilioni 20 kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kutoa mikopo ya nyumba.

Wakizungumza katika hafla hiyo, baadhi ya wawakilishi wa taasisi hizo wamesema msaada huo ni kichocheo kikubwa cha upatikanaji wa mitaji, upanuzi wa huduma za kifedha, na uboreshaji wa fursa za ajira, hasa kwa vijana kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Uwekezaji huu ni sehemu ya mkakati mpana wa EADB wa kuimarisha mifumo ya kifedha katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na kuchochea maendeleo endelevu ya kikanda.

















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...