Ecobank Tanzania imezindua rasmi tawi lake jipya katika eneo la Kariakoo, ikiwa ni hatua muhimu ya kusogeza huduma za kifedha karibu na kitovu kikuu cha biashara nchini. Tawi hilo lipo katika mtaa wa Mkunguni na Lumumba, ambapo limepokelewa kwa furaha na wafanyabiashara wa eneo hilo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, Severini Joseph Mushi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi amepongeza hatua ya Ecobank kurudi Kariakoo na kusema ni jambo la faraja kwa wafanyabiashara. 

“Tawi hili litachochea shughuli za uchumi na kuimarisha maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla,” alisema Mushi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa  Ecobank Tanzania, Dkt. Charles Asiedu amesema dhamira ya benki hiyo ni kuwafikia wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa kwa kutoa huduma za kisasa, rahisi na salama. Benki hiyo, ambayo inatoa huduma katika zaidi ya nchi 33 barani Afrika, imeahidi kusaidia wafanyabiashara wa Kariakoo kuunganishwa kimtandao na masoko mengine ya bara hili.

Katika hafla hiyo, Ecobank pia ilitangaza kuwa hivi karibuni ilitunukiwa tuzo ya Benki Bora Barani Afrika kwa mwaka 2025 kutoka kwa jarida la Global Finance, ikithibitisha ubora na uimara wa huduma zake.

Huduma zitakazopatikana katika tawi la Kariakoo ni pamoja na kufungua akaunti binafsi na za kibiashara, mikopo ya biashara, malipo ya kielektroniki ya haraka na salama, uhamisho wa fedha ndani na nje ya nchi na huduma za kubadili fedha za kigeni.

Tawi litakuwa wazi kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi 12:00 jioni siku za kazi, na kuanzia saa 2:30 hadi 10:00 jioni siku za Jumamosi.

Kwa sasa, Ecobank ina matawi, ATM na mawakala katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza — ikiwa na lengo la kuwafikia Watanzania wengi zaidi ambao bado hawatumii huduma rasmi za kibenki.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, Severini Joseph Mushi (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi la Ecobank Tanzania eneo la Kariakoo ikiwa ni hatua muhimu ya kusogeza huduma za kifedha karibu na kitovu kikuu cha biashara nchini. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa  Ecobank Tanzania, Dkt. Charles Asiedu 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, Nd. Severini Joseph Mushi (katikati), Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa  Ecobank Tanzania, Dkt. Charles Asiedu na  Mwakilishi wa  TWCC  Tawi la Kariakoo Shukuruni Lukumbuho Mkondya (kulia) wakipiga makofi mara baada ya kuzindua  tawi la Ecobank Tanzania eneo la Kariakoo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, Severini Joseph Mushi akionesha kadi yake ya Ecobank mara baada ya kufungua akaunti kwenye benki hiyo wakati wa uzinduzi wa tawi la banki hiyo eneo la Kariakoo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, Severini Joseph Mushi akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la Ecobank Tanzania eneo la Kariakoo.
Mkurugenzi Mtendaji wa  Ecobank Tanzania, Dkt. Charles Asiedu akizungumza na wateja pamoja na wafanyakazi wa banki hiyo wakati wa uzinduzi wa tawi la Ecobank Tanzania eneo la Kariakoo.
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Samalu akitoa neno la ukaribisho wakati wa uzinduzi wa tawi la Ecobank Tanzania eneo la Kariakoo.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara kwa Wateja Wakubwa (Commercial Banking) Joyce Ndyetabura akizungumzia kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa wadau wateja wa Benki hiyo wakati wa uzinduzi wa tawi la Ecobank Tanzania eneo la Kariakoo.

Huduma zikiendelea kutolewa 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...