Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Madaba mkoani Ruvuma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Joseph Kizito Mhagama, amechukua fomu ya kuwania tena nafasi ya ubunge wa jimbo hilo kwa lengo la kuendeleza jitihada za kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Mhagama amekishukuru chama chake kwa kumpa nafasi ya kushiriki mchakato wa kuomba ridhaa ya kugombea, akibainisha kuwa CCM imeendelea kumuunga mkono tangu alipoanza safari ya kisiasa katika jimbo hilo, amesema kuwa chama kimekuwa kikikubalika Jimboni humo kutokana na utekelezaji mzuri wa ilani ya chama kwa vipindi viwili mfululizo.

Mhagama ameeleza kuwa kwa kipindi cha miaka kumi aliyotumikia wananchi wa Madaba, miradi mingi ya maendeleo imefanikishwa ikiwemo sekta za elimu, afya, maji na miundombinu, jambo linalompa sababu ya kuamini kuwa wananchi bado wanahitaji uongozi wa chama hicho  ili kuendeleza mafanikio hayo.

Ameongeza kuwa dhamira yake ya kuomba muhula wa tatu si kwa ajili ya maslahi binafsi bali ni kuendeleza yale ambayo tayari yameanza kufanyika, pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto mpya zinazowakabili wananchi. Amesisitiza kuwa maendeleo ya kweli hujengwa kwa mshikamano, uwazi na ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...