Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva amewaasa vijana wa Lindi kuweka juhudi na jitihada katika mambo wanayoyafanya ili kupata matokeo tarajiwa.
Mhe. Mwanziva ametoa nasaha hiyo, Juni 10, 2025 wakati wa mahafali ya wanafunzi waliohitimu Mafunzo ya Ufundi Stadi Ngazi ya Tatu katika Chuo cha VETA Lindi.
Mhe. Mwanziva ambaye alishiriki mahafali hayo kama mgeni rasmi alisisitiza vijana waliohitimu na wale wanaoendelea na masomo kuweka jitihaha kwa kuwa hakuna njia ya mkato kufikia mafanikio.
“Wewe ambaye umepata ujuzi wako, nenda ukaweke jihitada utapata matokeo. Wewe ambaye bado unaendelea na masomo, nenda ukafanye jitihada utapata matokeo.” alisisitiza Mwanziva
Pamoja na nasaha hizo, Mhe. Mwanziva amezipongeza Kampuni za Nishati za Kimataifa za Equinor Tanzania na Shell Exploration and Production Tanzania Ltd kwa kufadhili vijana 24 kwa mwaka 2024/25 kutoka Mkoa wa Lindi kusomea kozi mbalimbali chuoni hapo.
Kupitia ufadhili wa kampuni hizo, vijana hao wameweza kusomea fani mbalimbali zikiwemo umeme, ubunifu wa mavazi na teknolojia ya nguo, uchomeleaji na uungaji vyuma, viyoyozi na majokofu, ufundi magari, na uashi.
Kampuni hizo pia zimewezesha vitendea kazi kwa wahitimu hao kwa lengo la kuwasaidia kutumia ujuzi walioupata kujiajiri.
Mhe. Mwanziva aliwakabidhi wahitimu hao vitendea kazi hivyo mara baada ya kuwatunuku vyeti wakati wa mahafali.

Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva (kushoto) akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa Mafunzo ya Ufundi Stadi Ngazi ya Tatu kutoka Chuo cha VETA Lindi wakati wa mahafali yaliyofanyika Juni 10, 2025
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...