SHIRIKISHO la ngumi Tanzania (BFT) leo limeanza mashindano ya wazi ya ngumi ya ubingwa wa Taifa 2025. Katika ukumbi wa Manyara uliopo Tandale. Dar es
salaam.
Mashindano hayo yameanza leo kwa hatua ya kupitia nyaraka husika na kuwaandikisha wale wote watakaofuzu vigezo vya kushiriki mashindano hayo. Zoezi hili litaendelea leo hadi saa 8.00 Mchana.
Kesho kuanzia saa 3.00 Asubuhi hadi saa 5.00 zoezi hili litaendelea na kuanzia saa
6.00 Mchana hadi saa 8.00 Mchana kutakuwa na zoezi la kutayarisha ratiba itakayotuongoza katika mashindano hayo.
Uzito utakaoshindaniwa ni kama ifuatavyo:-
WANAUME. WANAWAKE
1. Minimumweight 48Kg 1. Minimumweight 48kG
2. Flyweight 51Kg 2. Light Flyweight 50Kg
3. Bantamweight 54Kg 3. Flyweight 52Kg
4. Featherweight 57Kg 4. Bantamweight 54Kg
5. Lightweight 60Kg 5. Featherweight 57Kg
6. Light Welterweight 63.5Kg 6. Lightweight 60Kg
7. Welterweight 67Kg 7. Light Welterweight 63Kg
8. Light Middleweight 71Kg 8. Welterweight 66Kg
9. Middleweight 75Kg 9. Light Middleweight 70Kg
10. Light heavyweight 80Kg 10. Middleweight 75Kg
11. Cruiserweight 86Kg 11. Light heavyweight 81Kg
12. Heavyweight 92Kg 12. Heavyweight 81+Kg
13. Super Heavyweight 92+Kg.
Hatua ya uchezaji ulingoni itaanza rasmi Jumatano ya tarehe 4 na fainali ya mashindano haya itakuwa Jumamosi ya tarehe 7/6/2025.
NB: HAKUNA BONDIA ATARUHUSIWA KUSHIRIKI MASHINDANO HAYA KAMA ATASHINDWA KUTUMA JINA KATIKA ZOEZI LA UANDIKISHAJI LINALOENDELEA LEO NA KESHO.
Makore Mashaga Katibu Mkuu- BFT.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...