MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam inatarajia kusikiliza maombi ya kuongeza muda wa kukata rufaa dhidi ya mfanyakazi wa benki Ibrahim Masahi aliyetuhumiwa kumjeruhi jirani yake kwa nyundo kisa kushtakiwa Serikali ya mtaa kwa kutililisha maji machafu, Julai Mosi 2025.
Masahi alikuwa akituhumiwa kwamba Januari 11, 2023 akiwa eneo la Mbezi Msakuzi ndani ya Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam alimpiga Deogratus Minja kwa nyundo na kumsababishia kupata madhara makubwa ya mwili mwake.
Hata hivyo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam baada ya kusikiliza kesi hiyo ya tuhuma za kujeruhi ilimuachia huru kutokana na kwamba upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha shtaka bila kuacha shaka lolote.
Kutokana na hukumu hiyo, upande wa Jamhuri waliwasilisha kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu hiyo iliyotolewa na Hakimu Mkazi Amos Rweikiza kwamba mshtakiwa katika ushahidi wake hakueleza jinsi alivyomtambua usiku wa tukio hilo.
Huku upande wa mashtaka kueleza kwamba waliweza kuthibitisha shtaka kwa sababu shahidi wao alieleza jinsi alivyomtambua mshtakiwa Masahi kwa kulikuwa na mwanga wa kutosha wa taa za nje.
Maombi hayo yatasikilizwa mbele ya Jaji Mfawidhi, Salma Maghimbi Julai Mosi, 2025 saa nne asubuhi. Mjibu wa maombi (Masahi) kupitia wakili wake wamewasilisha majibu ya maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Jamhuri (kiapo kinzani).
Awali, katika kesi ya msgingi Daktari Bingwa wa Mifupa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kitendo cha Mifupa (MOI), Joel Mwinza (44), aliieleza kwamba alimpokea Minja lakiwa na majeraha kichwani, mgongoni, mkononi na pia kuna sehemu alikuwa amechanika kisogoni, kwa hiyo alitumia mashine ya X-ray na CT Scan kumchunguza mwili wake.
Katika ushahidi wake, Minja alidai kuwa tarehe hiyo saa mbili na nusu usiku alikuwa akipita nje ya geti la jirani yake Masahi, alimkuta kijana wa jirani huyo, baada ya kumuona alizungumza kwa kilugha kwa sauti kubwa ambae yeye hakuielewa.
"Ghafla kijana alikuja mbele yangu akanizuia nisipite, mara geti likafunguliwa akatoka Masahi akanihoji kwamba mimi ni kama nani na kwenda kumshitaki Serikali za Mitaa, sikumjibu chochote kijana wake akanipiga ngumi,"
"Nilimgeukia jirani yangu ili amuonye kijana wake, lakini na yeye aliinua shati lake juu akatoa nyundo akanipiga nayo kichwani baada ya kupata maumivu makali nilianza kukimbia huku nikipiga kelele za kuomba msaada,"amedai Minja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...