WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhwan Kikwete Nimeongoza Uzinduzi wa Maonyesho ya Ajira ya Nne (4) ya Tanzania na China yaliyofanyika katika Viwanja vya Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar-Es-Salaam , Dar Es Salaam.

Maonyesho hayo ambayo yanalenga kutangaza na kuwaunganisha Vijana wahitimu na wenye ujuzi Watanzania na makampuni ya Kichina yanayofanya kazi Nchini Tanzania.

Maonyesho hayo ambayo yanalenga kuwaunganisha vijana wa Kitanzania na fursa za Ajira nimeyafungua kwa kuwakumbusha umuhimu kuenzi ushirikiano uliopo wa nchi zetu mbili na hatua mbalimbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Dr. Samia Suluhu Hassan kutatua changamoto ya ajira nchini. Maonyesho haya yanataraji kutoa fursa za Ajira zaidi ya ajira 2000.

Kikwete amesema maonesho hayo ni kati ya hatua za serikali ya Awamu ya Sita katika kutatua changamoto ya Ajira nchini, ambapo kupitia maonesho hayo makampuni ya China yanayofanya kazi hapa nchini yanaonesha mahitaji yao ya ujuzi wanaohitaji ili vijana wakitanzania weweze kuchangamkia fursa hizo.

Hivyo vijana wenye sifa za mahitaji ya makampuni hayo kufuatia makubaliano baina ya serikali zetu katika kufikia maendeleo endelevu ambayo nchi yetu itafaidika katika shughuli za makampuni hayo nchini na kuwapa nafasi vijana wazawa wenye sifa wanazohitaji.

Katika hatua nyengine nimewahakikishia watanzania kuwa serikali kupitia ofisi hiyo itaendelea kuratibu kwa tija masuala ya ajira nchini huku tukisimamia maslahi mapana ya Watanzania kqma ilivyoelekezwa nq sheria, sera na miongozo ya Ajira na Kazi na maono yq Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara wa Nchini China kwa Upande Wa nchi ya Tanzania,Juma Sharobaro amesema Maonesho hayo yanayolenga kutoa Ajira zaidi ya 1000 hadi 2000 Kwa Vijana Wakitanzania.

"Vijana Watakaofanikiwa Kupata Ajira ni wale ambao walifata vigezo na Masharti ikiwemo kujisajiri mtandaoni ambao mapema Ubalozi wa China Walifungua Nafasi na Kuwapa Fursa Vijana Kujisajili ."


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...