Mhandisi na kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jafari Iddy Fadhili Hegga ( pichani kushoto) amechukua na kurudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki.

Awali, Mhandisi Jafari alikabidhiwa fomu na katibu wa CCM wilaya comrade Michael Bundala na kufanikiwa kuirudisha.

Anatarajiwa kuwa miongoni mwa wagombea wanaowania nafasi hiyo inayoshikiliwa kwa sasa na Mbunge aliyemaliza muda Hamis Taletale ( Babu Tale)

Mhandisi Jafari amesema ameguswa kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo na kuwaletea maendeleo kwa haraka kwa kushirikiana na viongozi wa chama jimboni humo pamoja na Serikali.

" Nikiwa kijana mwenye nguvu na kubobea katika mikakati ya kuleta maendeleo kwa kushirikiana na wananchi nimeona wakati umefika wa kuwa mtumishi wa watu wa jimbo hili,"

" Hivyo, naomba ridhaa ya chama changu na wananchi kunipokea kwa mikono miwili ili tujiletee maendeleo ya haraka,", amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...