Namtumbo_Ruvuma.
Serikali inatarajia kuanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma, unaotarajiwa kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 1.4 hadi milioni 3.57 kwa siku na kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi kutoka asilimia 58 iliyopo sasa hadi asilimia 95.
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Namtumbo (NAUWASA), Mhandisi Francis I. Meddah alisema kuwa mradi huo unatekelezwa chini ya usimamizi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuboresha huduma za maji kwa wananchi kufatia maono ya Rais ya kumtua mama ndoo kichwani.
Mradi huo utahusisha ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita milioni moja, ununuzi na ulazaji wa mabomba yenye kipenyo cha kati ya inchi 6 hadi 16 kwa umbali wa mita 30,000. Pia, ujenzi wa banio (inteki) katika mto Libula na upanuzi wa chanzo cha maji cha mto Likiwigi vilivyopo kijiji cha Libango ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo.
Kazi nyingine ni pamoja na ununuzi na ufungaji wa dira za malipo ya kabla (prepaid meters), ujenzi wa jengo la ofisi na uzio wake, pamoja na ununuzi wa kompyuta, samani, gari aina ya Toyota Hilux na pikipiki sita kwa matumizi ya ofisi.
Mradi huo mkubwa wa maji wenye thamani ya Shilingi bilioni 6.6. Mradi huu unalenga kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Mji wa Namtumbo na unasimamiwa na wakandarasi wawili; M/S GOPA Contractors (T) Ltd kwa kazi za ujenzi, na M/S Pipe Industry Co. Ltd kwa kazi za usambazaji wa mabomba.
Amesema Watendaji wa kata na vijiji vilivyo kwenye maeneo ya mradi wamealikwa kushiriki ili kwenda kuutambulisha mradi kwa wananchi wao na kuwaambia kuwa mradi huo hautatoa fidia kwa maeneo yatakayopitiwa na mabomba au miundombinu mingine, kwani kazi zitafanyika kwenye maeneo ya pamoja.
Mradi huo unatarajiwa kunufaisha wakazi wapatao 45,902 katika maeneo ya Namtumbo Kati, Minazini, Kidugaro, Bomani, Lusenti, Mitalulaya, Magereza, Ushirika A na B, Uyaoni, Kisutu, Tembo, Tigotigo, Nasuli, Tanesco, Gongo la Mboto na Changarawe.
Kwa sasa, NAUWASA huzalisha lita milioni 1.5 kwa siku huku mahitaji halisi yakiwa ni lita milioni 3.5, na huduma ya maji safi mjini Namtumbo inapatikana kwa asilimia 58 pekee. Changamoto nyingine ni uchakavu wa miundombinu, uwezo mdogo wa matenki ya kuhifadhia maji, ukosefu wa mtandao wa mabomba kwenye maeneo mengi ya mji wa Namtumbo na ukosefu wa jengo la ofisi ya mamlaka hiyo.
Mhandisi Meddah alisema usanifu wa mradi huu umezingatia mahitaji ya sasa na ya baadae kwa kipindi cha miaka 20 hadi mwaka 2045, Wizara ya maji ilitoa kibali cha kutangaza zabuni ya mradi huo ili kuwapata Wazabuni wa kutekeleza mradi na utekelezaji rasmi utaanza mara baada ya kusainiwa kwa mikataba na upatikanaji wa msamaha wa kodi ya VAT.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Ngollo Malenya amepongeza hatua hiyo muhimu, akibainisha kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha huduma za maji zinaboreshwa kwa wananchi wa maeneo ya vijijini na mijini. Amehimiza wananchi kutoa ushirikiano wa karibu kwa mkandarasi ili kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Aidha, DC Ngollo ametoa wito kwa viongozi wa mitaa na vijiji kushirikiana na NAUWASA katika kusimamia utekelezaji wa mradi huo, akisisitiza kuwa maji ni huduma ya msingi na haki ya kila Mtanzania.
Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, wananchi wa Namtumbo, pamoja na wadau wa maendeleo waliokuja kushuhudia hatua hiyo muhimu ya uboreshaji wa huduma za kijamii.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...