Na Jane Edward Arusha

Katika kuendeleza jitihada za mageuzi ya sekta ya elimu nchini, Serikali imezindua rasmi awamu ya pili ya ugawaji wa vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa shule za sekondari zaidi ya 400 kote nchini.

Hafla ya uzinduzi huo imefanywa na Naibu waziri Tamisemi Zainabu Katimba katika shule ya sekondari ya Arusha na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu ikiwemo wazabuni wa Vifaa vya TEHAMA TanzTech.

Ambapo Mheshimiwa Zainab amesisitiza juu ya dhamira ya serikali kuwekeza katika elimu ya kidijitali kwa ajili ya kuongeza ubora wa ufundishaji na ufaulu kwa wanafunzi.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, serikali tayari imetumia zaidi ya shilingi bilioni 18 kufanikisha mradi huu, ambao kwa ujumla wake umewezesha shule zaidi ya 500 kupokea vifaa vya TEHAMA.

Amesema kuwa Hii ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya sekondari nchini ujulikanao kama SEQWIP (Secondary Education Quality Improvement Project), ambao hadi sasa umeshanufaisha zaidi ya shule 6,000.

Dkt Emanuel Shindika Mkurugenzi wa usimamizi wa elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI anasema usimamizi makini wa mradi huo na kuwataka walimu kuhakikisha vifaa vyote vinakabidhiwa kwa walengwa kwa wakati na kwa utaratibu mzuri.

"Vifaa hivi vinapaswa kutunzwa kwaajili ya mafunzo na kujifunza ili kuweza kuongeza kiwango cha ufaulu katika masomo hayo ya Tehama kwa wanafunzi wetu"Alisema Shindika

Aidha, shule zimehimizwa kuimarisha usalama wa madarasa ya TEHAMA, kuhakikisha vifaa vinatunzwa kwa uangalifu na kuweka mazingira safi na rafiki kwa matumizi ya teknolojia, ikiwemo kuweka mapazia ili kudhibiti vumbi ambalo linaweza kuharibu vifaa hivyo.

Faida kuu zinazotarajiwa kutokana na uwekezaji huu ni pamoja na:

Kuwezesha wanafunzi kujifunza kwa njia ya kidijitali na kuona maarifa kwa uhalisia zaidi.

Uwezeshaji wa vipindi vya mtandaoni, hali itakayosaidia kupunguza gharama za ufundishaji.

Kuongeza ufaulu kwa wanafunzi kupitia mbinu bunifu za kisasa.

Kuwajengea walimu uwezo wa kufundisha kwa kutumia teknolojia kwa mujibu wa miongozo ya serikali na mabadiliko ya kisera.

Kwa upande wake Mwalimu Robart Msigwa ambaye ni mratibu msaidizi wa mradi wa SEQWIP anasisita kuwa walimu kote nchini kuhakikisha wanatumia vifaa hivi kwa weledi, wakizingatia malengo ya sera ya elimu ya taifa, huku wakiwa daraja la kufanikisha mabadiliko ya kweli katika elimu ya Tanzania.

Mradi huu unatarajiwa kuwa chachu ya kuibadilisha elimu ya sekondari kuwa ya kidijitali, jumuishi na yenye kumwandaa mwanafunzi wa Kitanzania kukabiliana na ushindani wa soko la ajira la ndani na kimataifa katika kipindi hiki ambacho teknolojia imekuwa zaidi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...