Na Mwandishi Wetu.Ngorongoro,Arusha.

Benki ya NMB kupitia kampeni yake ya NMB Kijiji Day imefanya shughuli mbalimbali za kijamii katika tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha, zikiwemo michezo, elimu ya fedha, na kuhamasisha vijana kuhusu fursa zilizopo kupitia michezo na ujasiriamali.

Tukio hilo lilifanyika katika uwanja wa WASSO ambapo wananchi walishiriki katika michezo mbalimbali kama jogging na mpira wa miguu. Mechi ya soka kati ya timu ya Loliondo na Serengeti ilipamba tamasha hilo, na timu ya Serengeti iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Mbali na michezo, NMB ilitoa elimu ya fedha kwa vikundi vya ujasiriamali, ikiwalenga wananchi wa Ngorongoro, ambapo zaidi ya watu 150 walifikiwa na kufundishwa kuhusu mbinu za kuhifadhi fedha, kupata mikopo, na kukuza biashara zao kupitia huduma za kifedha za benki hiyo.

Afisa Masoko wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini wa, Bw. Innocent Mwanga, alisema benki hiyo itaendelea kushirikiana na jamii katika kuimarisha michezo na kuinua uchumi wa wananchi kupitia elimu ya fedha.

Katika tukio hilo, vijana wa Ngorongoro walitoa wito kwa wadau na wapenzi wa soka wilayani humo kuanzisha ligi rasmi zitakazosaidia kuinua vipaji vya michezo miongoni mwa vijana, kuwaepusha na vishawishi, na kuwafanya wapende kushiriki katika shughuli za maendeleo kupitia michezo.

Kampeni ya NMB Kijijini Day imeendelea kuwa jukwaa la kipekee la kuunganisha huduma za kifedha, michezo na elimu ya jamii, ikiwafikia wananchi moja kwa moja vijijini.

Kwa Upande wao Wakazi wa Ngorongoro akiwemo Philemon Molel wameipongeza benki ya NMB kwa kuja na ubunifu wa kuwafikia wananchi wa vijijini na kuwapatia elimu ya fedha ili waweze kuchangamkia fursa zinazotokana na uwepo wa huduma za kifedha kwenye maeneo yao.














Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...