TANZANIA imepiga hatua kubwa na thabiti kuelekea uhuru wake kamili wa kiuchumi kwa kufadhili na kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu ya kiuchumi kwa kutumia fedha zake za ndani pekee.

Mbali na Mradi wa bwawa la kuzalisha umeme la JKNHEP liliogharamiwa kwa zaidi ya shilingi trilioni sita, ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi, mradi uliogharimu shilingi bilioni 718 kutoka kwenye bajeti ya serikali ni kielelezo kingine cha mafanikio hayo.

Kauli hiyo imetolewa na Mheshimiwa Profesa Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, alipokuwa akizungumza kwenye Kongamano la Mwananchi Jukwaa la Fikra liliondaliwa kwa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, likijadili mada isemayo, ‘Kujenga Madaraja Kujenga Taifa: Miundombinu kama Kichocheo cha Ukuaji Jumuishi.’

Waziri Profesa Mkumbo ameeleza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi si tu ishara tosha ya uhuru wa kiuchumi, bali pia utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuifungua nchi.

Daraja hili muhimu linatarajiwa kuchochea kwa kiasi kikubwa shughuli za uwekezaji na biashara nchini, likiimarisha usafirishaji wa bidhaa muhimu kama samaki na madini. Aidha, litachangia katika kukuza biashara na nchi jirani, na hivyo kuimarisha uhusiano wa kiuchumi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aidha, ujenzi wa daraja hilo unawakilisha nguzo muhimu katika kutekeleza maono ya Dira mpya ya Taifa ya Maendeleo 2050, ambayo inalenga kufikia Uchumi wa Daraja la Kati Juu kwa kukuza Pato la Taifa kufikia dola za Marekani trilioni Moja.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo (kulia), akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, Mlimani City, Dar es Salaam, Juni 22, 2025. Mawaziri hao walikuwa tayari kushiriki Jukwaa la Fikra lililojadili miundombinu kama kichocheo cha ukuaji wa taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...