Na Emmanuel Mbatilo, Michuzi Tv
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ongezeko la majukwaa ya habari kupitia mitandao na majukwaa ya kidijitali limeleta mapinduzi makubwa ya upatikanaji wa taarifa nchini, ambapo kwa sasa habari nyingi zinapatikana kwa urahisi kupitia simu janja na vifaa vingine vya kielektroniki.
Akihutubia Bunge la 12 Jijini Dodoma wakati wa kuhitimisha shughuli zake leo, Rais Samia amesema Serikali imetoa leseni kwa vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo magazeti na majarida 356, vituo vya redio 247, televisheni 68, redio na televisheni za mtandaoni 325 pamoja na blogu 72.
"Mpaka sasa tuna magazeti ya kila siku na kamwe Serikali haijafanya uhakiki wa habari kabla hazijachapishwa au kuandikwa. Tunafanya hivi tukiamini waandaaji wa maudhui haya ni watu wenye weledi wa kutosha," alisema Rais Samia, akiweka wazi dhamira ya Serikali katika kulinda na kuendeleza uhuru wa vyombo vya habari.
Aidha, alieleza kuwa Serikali imefanya marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 pamoja na kanuni zake ili kuboresha mazingira ya kazi kwa waandishi wa habari. Vilevile, alitaja kuanzishwa kwa Tuzo za Samia Kalamu Awards kama sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wa waandishi wa habari za maendeleo.
Hata hivyo, Rais Samia alisisitiza kuwa pamoja na kuendeleza uhuru wa habari, Serikali haitasita kuchukua hatua pale ambapo uhuru huo utatumiwa vibaya, kutishia amani ya nchi au kukiuka sheria, maadili, mila na desturi za Watanzania.
“Tutalinda uhuru wa habari lakini si kwa gharama ya kuvuruga usalama wa jamii yetu,” alisisitiza.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...