Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya, Shirika la Maendeleo la Mitaji la Umoja wa Mataifa (UNCDF) na wadau wengine wa maendeleo, leo imezindua rasmi Mkakati wa Mawasiliano wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia pamoja na Kampeni ya Uhamasishaji kuhusu nishati safi katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Uzinduzi huu ni hatua muhimu katika juhudi za taifa kufikia asilimia 80 ya matumizi ya nishati safi kwa upishi ifikapo mwaka 2034, kwa mujibu wa malengo yaliyowekwa kwenye Mkakati wa Taifa wa Upishi Safi 2024–2034.
Hafla hiyo ya uzinduzi ilihudhuriwa na zaidi ya washiriki 250, wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali, mamlaka za serikali za mitaa, wawakilishi wa mashirika ya maendeleo, wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs), taasisi za kifedha, vyuo vya elimu ya juu na taasisi za utafiti, wanahabari, na mashirika ya kiraia.

Ushiriki wao unaashiria mshikamano wa kitaifa katika kutambua kuwa nishati safi ni muhimu si tu kwa afya ya jamii, bali pia kwa mazingira, ukuaji wa uchumi, na usawa wa kijinsia.
Akitoa hotuba kuu ya uzinduzi, Mgeni Rasmi Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, alisisitiza umuhimu wa kampeni ya uelimishaji katika kufanikisha malengo ya kitaifa ya nishati safi:
“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameweka nishati safi kuwa kipaumbele cha kitaifa katika maendeleo. Uzinduzi huu wa Mkakati wa Mawasiliano na kampeni ya kitaifa unaonesha dhamira yetu ya kuwafikia Watanzania wote ili kuleta mabadiliko. Bila uelewa, hakuna mabadiliko. Kampeni hii ni wito kwa kaya, jamii, na taasisi kukumbatia matumizi ya nishati safi na ya kisasa.”
Akiendelea kufafanua juu ya dira ya kampeni hiyo, alisema:
“Kampeni ya uhamasishaji itatekelezwa kwa awamu ikianza na ujumbe kupitia vyombo vya habari kitaifa, ikifuatiwa na mikakati ya uhamasishaji katika jamii, elimu kupitia shule, na maonesho ya masoko. Lengo letu ni kujenga mazingira rafiki ambapo maarifa haya yatachangia kuleta mabadiliko ya tabia, na mabadiliko hayo kuleta mahitaji ya nishati safi.

Hii ni safari ya miaka kumi inayoanza leo, na kila kata na kijiji kitakuwa sehemu ya kampeni hii. Tumejipanga kushirikisha viongozi katika ngazi zote ili ujumbe wa nishati safi uweze kuwafikia Watanzania wote.”
Kampeni ya kitaifa ya miaka kumi ya uhamasishaji itatumia njia mbalimbali za mawasiliano kuwafikia wananchi wengi nchini. Itajumuisha vyombo vya habari kama redio, televisheni, magazeti; itahusisha ushirikishwaji wa jamii kupitia matukio ya moja kwa moja, maonesho ya barabarani, na programu katika shule; pia itatumia majukwaa ya kidigitali ikiwemo mitandao ya kijamii, ujumbe mfupi wa simu (SMS), na programu za simu.

Aidha, kutakuwa na ushirikiano na viongozi wa dini, walimu, taasisi za kijamii, na watu wenye ushawishi katika jamii. Mbinu hii shirikishi inalenga kuleta ushiriki wa kudumu wa wananchi, kubadili mitazamo, na kuongeza matumizi ya teknolojia za nishati safi majumbani na katika jamii.
Akizungumza kwa niaba ya Umoja wa Ulaya, Bw. Lamine Diallo, Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Asili, alisisitiza umuhimu wa elimu jumuishi na upatikanaji wa taarifa:
“Uelewa si anasa ni msingi wa mabadiliko. Umoja wa Ulaya unajivunia kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kampeni hii muhimu. Lengo letu la pamoja ni kuhakikisha kuwa familia zote, bila kujali eneo au kipato, zinaelewa faida za kiafya, kimazingira, na kiuchumi za nishati safi, na kuwa na fursa ya kupata suluhisho bora na nafuu. Mkakati huu wa mawasiliano ni nyenzo muhimu kuhakikisha mabadiliko haya ni jumuishi na endelevu.”
Bw. Imanuel Muro, Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Fedha kutoka UNCDF, alielezea faida za mkakati huu kwa mifumo ya soko na uimara wa jamii:
“Mawasiliano ni chombo cha kuwajengea watu uwezo. Mkakati huu hauishii kwenye kuelimisha tu bali unanuia na kubadilisha masoko, kukuza biashara zinazohusika na nishati safi ya kupikia, na kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi sahihi na yenye tija. Mafanikio ya kampeni hii yatapimwa kwa matokeo halisi katika maisha ya kila siku ya watu katika jamii zetu za kitanzania.”
Uzinduzi huu ni mwanzo wa harakati za kitaifa za kuhakikisha upatikanaji wa nishati safi kwa wote, hatua muhimu kuelekea Tanzania yenye afya bora, mazingira safi, na maendeleo jumuishi.

Mhe. Doto Mashaka Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati (katikati) akizidindua mkakati wa Taifa wa Mawasiliano wa Nishati Safi ya Kupikia mkoani Dodoma. Kulia kwake ni Lamine Diallo, mwakilishi kutoka Umoja wa Ulaya (EU), wa pili kushoto ni Mhe. Judith Kapinga (Naibu Waziri wa Nishati), wa Kwanza kulia ni Angellah Kairuki (Mshauri Maalumu wa Raisi katika Masuala ya Nishati Safi ya Kupikia na Maendeleo ya Jamii) na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary S. Senyamule.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...