Na Mwandishi wetu, Simanjiro
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Queen Cuthbert Sendiga ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kwa kupata hati safi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali CAG kwa mwaka wa fedha wa 2023 hadi Juni mwaka 2024.
baadhi ya wanasiasa waliodhani kuwa ataondoka wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 watambue kuwa bado yupo sana na atapiga kura kwenye mkoa huo.
Baadhi ya viongozi wa kisiasa wamekuwa wanawatangazia watu kuwa Sendiga ataondoka kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu na kuteuliwa kiongozi mwingine wa mkoa huo.
Sendiga ametosema pongezi hizo kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, cha kujadili taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG kwa mwaka wa fedha wa 2023 hadi Juni 2024 ambapo imepata hati safi.
Sendiga ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kwa kupata hati safi kwenye taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024.
Hata hivyo, ameitaka Halmashauri hiyo wahakikishe kwamba wamefunga hoja zinazotakiwa ili waondokane nazo kuliko kuwa na hoja zinazojirudia.
"Wakuu wa idara na vitengo kila mmoja ahakikishe anawajibika kupitia nafasi yake na hoja iliyoelekezwa kwake na watumishi waliosababisha hoja hizo wachukuliwe hatua," amesema Sendiga.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Gracian Max Makota amesema kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 Halmashauri hiyo ilikuwa na hoja 42.
Makota amesema hoja 28 ziliibuliwa na kutolewa mapendekezo kwa mwaka 2023/2024 na hoja 14 ni za kipindi cha mwaka wa fedha wa 2017/2018 hadi mwaka 2022/2023.
Amesema halmashauri hiyo imefanikiwa kufunga hoja 15 kati ya hoja 42 baada ya CAG kuhakiki na kuridhia majibu yaliyowasilishwa na halmashauri hiyo.
"Zimebaki hoja 27 ambazo hazijaridhiwa kufungwa, kati ya hizo hoja 11 ni za kipindi cha sasa 2023/2024 na hoja nne ni za kipindi cha nyuma," amesema Makota.
Ametoa shukrani za dhati kwa mwenyekiti wa halmashauri, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mbunge, madiwani na wadau mbalimbali hadi kuwezesha halmashauri hiyo kupata hati safi.
"Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro inaahidi kuendelea kufanya vizuri kwa kipindi kijacho ili kuweza kupata hati safi mfululizo," amesema Makota.
Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Fakii Raphael Lulandala amewapongeza madiwani wa halmashauri hiyo kwa kumpa ushirikiano wa kutosha katika kipindi chao.
Lulandala amewataka madiwani hao kupitia kipindi hiki ambacho wanatarajia kumaliza muda wao wakayazungumze kwa wananchi maendeleo yaliyopatikana kupitia serikali ya awamu ya sita.
"Madiwani mkayaseme mazuri yote yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na pia mkayazungumze na ya kwenu, natarajia mtarudi kupitia uchaguzi kwani mmefanya kazi," amesema Lulandala.
Diwani wa kata ya Mirerani, Salome Nelson Mnyawi amemshukuru Sendiga kwa kusimamia vyema maendeleo kwani eneo lake ni miongoni mwa waliopata miradi ikiwemo kituo kipya cha afya cha Tanzanite.
Diwani wa kata ya Endiamtu Lucas Zacharia amempongeza mkuu wa mkoa wa Manyara, kwa namna anavyotekeleza vyema wajibu wake kwa kuitumikia jamii.
Diwani wa kata ya Naisinyai Taiko Laizer amesema anamshukuru mkuu huyo wa mkoa kwa namna alivyoshirikiana na madiwani katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana.
Diwani wa kata ya Loiborsoit, Siria Baraka Kiduya amempongeza mkuu huyo wa mkoa kwa namna alivyosimama kidete kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwenye kata mbalimbali kupitia miradi.
Diwani wa kata ya Msitu wa Tembo, Kaleya Mollel amesema anampenda sana mkuu huyo wa mkoa kwani ni mama mpenda maendeleo na mwenye msimamo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...