NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), kupitia Mamlaka yake ya Uwekezaji (ZIPA), imeishukuru, kuipongeza kuitunukia Cheti Maalum Benki ya NMB kwa ‘kulibeba mabegani’ kwa udhamini mnono na ushiriki wa Kongamano la Uwekezaji Zanzibar 2025, lililofungwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi.
Kongamano la Uwekezaji Zanzibar (ZIS), limefanyika kwa siku mbili kwenye Eneo Huru la Uwekezaji la Micheweni, Pemba, likiwakutanmisha pamoja wawekezaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, lililofanyika kwa udhamini wa NMB chini ya kaulimbiu ya ‘Ni Wakati wa Pemba,’ likiangazia fursa za uwekezaji zilizopo kisiwani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na Ofisi ya Raias Zanzibar kwa ajili ya wawekezaji walioshiriki ZIS 2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Saleh Saad Mohamed, alisema udhamini na ushiriki wa NMB, unaakisi imani waliyonayo kwa SMZ na taasisi zake
“Nitumie nafasi hii kuwashukuru wenzetu wa NMB Bank kwa kuendelea kutusapoti ZIPA, lakini pia tunawashukuru kwa kuendelea kutuamini na kuamini kuwa Zanzibar ni sehemu sahihi ya wao kuwekeza na kusapoti uwekezaji unaofanywa na Serikali ya Mapinduzi.
“Pia shukrani hizi ni kutokana na ukweli kuwa, NMB imeendelea kuamini kuwa ZIPA ni marafiki wao wa karibu daima, wameendelea kutuunga mkono na kutuwezesha katika maendeleo ya mifumo na masuala mengine tunayoshirikiana nao kufanya pamoja kwa maendeleo na ustawi wa Zanzibar na Wazanzibar.
“Kwa niaba ya SMZ na ZIPA, nitumie nafasi hii kumshukuru Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna na wafanyakazi wote kwa kuendelea kutuunga mkono, kutusaidia, ambapo siku zote NMB imekuwa bega kwa bega na SMZ, imekuwa bega kwa bega na ZIPA.
“Tunaamini kupitia uwezeshaji wa NMB, tutakuwa na kongamano kubwa, bora la lenye washiriki wengi zaidi tutapolifanya tena mwakani 2026,” alibainisha Saleh, ambaye Mamlaka yake iliratibu Kongamano hilo lililoanza kwa Matembezi ya Hisani, upimaji afya bure, Maonesho ya Uwekezaji na Chakula cha Usiku.
Akizungumza mbele ya Rais wa Zanzibar Dk. Mwinyi, Mkuu wa Kitengo cha Miamala ya Benki ya NMB, Bi. Linda Teggisa, aliishukuru SMZ na ZIPA kwa kuamini katika ushirikiano baina yao na kuwapa fursa ya kuchangamana na wawekezaji wazawa na wageni na kuwaonesha fursa za kukuza Uchumi wa Buluu.
Akiahidi ushirikiano endelevu na SMZ na taasisi zake, Bi. Linda alisema Kongamano la Uwekezaji Zanzibar lilikuwa ni zaidi ya jukwaa bora liklilowawezesha kuonesha nguvu, uimara na ubora wa huduma zao kwa kada ya wawekezaji na kuwataka kuifikiria benki hiyo, watapowaza kufanya uwekezaji wao ili kujenga Uchumi Shindani.
“NMB tunashukuru kutupa nafasi ya kushirikiana kufanikisha Kongamano la Uwekezaji Zanzibar. Sisi kama NMB tumetumia vema fursa hii kuhakikisha kwamba tunaweza kuonesha uwezo wetu, fursa zetu na huduma rafiki kwa wawekezaji tulizonazo wanazoweza kupata wakiwa nchini ama nje ya nchi.
“Tumeonesha masuluhisho tuliyonayo kama benki kinara nchini, lengo likiwa ni kudumisha ushirikiano sio tu na wawekezaji wazawa, bali hata wawekezaji wa kigeni, ambao wanaweza kuja Tanzania na kupata suluhisho zote muhimu kwa ustawi na maendeleo ya uwekezaji wao,” alibainisha Bi. Linda.
Aidha, aliongeza kuwa ushirikiano baina yao na SMZ utaendelea kudumu, na kwamba: “Tumeshirikiana na ZIPA katika maeneo mengi muhimu, ikiwemo ujenzi wa mfumo imara wa ‘Zanzibar Investment Electronic Window,’ ambao unatoa fursa ya kila upande kupata taarifa muhimu inazohitaji kutoka upande wa pili.
“Zanzibar Investment Electronic Window’ ni sehemu ambapo wawekezaji wanaweza kupata ‘certificate’ kutoka ZIPA, ambao nao wanaweza kupata taarifa mbalimbali kuhusus Uwekezaji na Wawekezaji. Tunaamini kuwa sisi kama benki inayoongoza, tunaweza kuendelea kushirikiana na SMZ kuhakikisha uchumi wa kidigitali unawezekana,” alisema Bi. Linda.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...