Na.Vero Ignatus Arusha
Imeelezwa kuwa ili uweze kupata maziwa ya kutosha kwenye viwanda lazima kuwepo na elimu na mitaji, sambamba na kuwepo na mbegu bora za mifugo kwa wafugaji waweze kufuga kisasa ,kudhibiti magonjwa kuboresha malisho Ili kuongeza tija .
Steven Maiko mkurugenzi wa Uzalishaji na maendeleo ya masoko ambapo amemuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, amesema wakati wa ufungaji wa mradi Jumuishi wa kuboresha maisha ya wafugaji wadogo kupitia maziwa ( DNA-BILD) Jijini Arusha uliofadhiliwa na serikali ya sweeden wa tahaman za dola za kimarekani Mil 1.4 ulioanza 2022 na unafungwa june 2025 ambao umetekelezwa kwa takribani miaka 3 .
Amesema kuwa Mradi huo unaendana na mipango ya serikali sera na mkakati kwasababu miongoni mwa malengo ya sekta ya mifugo ambayo ni sekta ya uchumi ni kuchangia malighafi ya viwanda kuongeza ajira kipato cha wafugaji, ,hivyo wana mpangomkakati wa sekta ambacho umeonyesha kiasi cha uzalishaji ni kidogo ukilinganisha na mahitaji,hivyo wakiangalia tathmini ya mradi huu unaaomaliza muda wake umesaidia kwani inaonyesha ndani ya miaka 3 kipato cha wafugaji kimeongezeka,elimu ,mifugo bora na kupata maziwa wenye ubora na kupunguza hasara za kuharibika kwa maziwa wakati wa usindikaji
‘’Kwahiyo mradi huu umejikita kwenye mikoa ya nyanda za juu kaskazini yenye fursa ya uzalishaji wa zao la maziwa na umeweza kuongeza elimu ,mitaji, kwa wasindikaji,kuongeza tija,kulima majalni ya malisho mamzuri pamoja na kufanya uhifadhi,wamepata vitendea kazi, wamepata pia elimu kupitia mashamba darasa namna ya kuzalisha kwa tija,mradi pia umeangazia maeneo ya kisera kwamaana ya kuboresha maeneo ya kufanya biashara,ukiangalia kulikuwa na changamoto ya uingizaji wa mbegu zinazotakiwa na wafugaji,vifungashio tumesikia mradi huu umewezesha wawekezaji mbalimbali ‘’
Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Prof.George Mtani Msalya amesema kuwa hadi sasa bado kuna upungufu wa maziwa kwani hadi sasa wanazalisha lita bil.4.01 kwa takwimu za Mwaka 2024,ambapo wanahitaji kufikia lita bil 13 miaka michache ijayo ili kufikia utoshelevu wa maziwa nchini
Aidha ametaja changamoto ambazo zinachangia kuwepo kwa uzalishaji mdogo wa maziwa nchini ikiwa ni pamoja na washauri ni wachache,uwekezaji wa vyakula vya mifugo hali ya hewa,ng’ombe ambao siyo bora japokuwa Tanzania ni nchi ya pili kwa wingi wa mifugo Barani Afrika,zaidi ya asilimia 90%ni mifugo ya kienyeji ambayo uzalishaji wake ni mdogomdogo.
‘’Kwasababu tunazo changamoto tunahitaji nguvu za ziada za pamoja kuweza kutatua changamoto hii ili tuweze kupata maziwa mengi kwasababu maziwa ni afya ni chakula na tunayahitaji ili kuondoa utapiamlo nchini,kwani serikali inafanya kwa upande wake wadau wanafanya kwa upande wao na miogoni mwa wadau tunao kundi zuri la wadau wa maendeleo mashirika ya kimataifa na mashirika ya ndani ambayo yamewekeza na wanafanya shughuli zao katika tasnia ya maziwa,nawaomba wasindikaji, wafugaji mliopata mafunzo mkayatumie kwa manufaa na kuleta tija katika Taifa’’alisema.
Amewashukuru wadau hao kwani wamekuwa nchini kwa miaka 35 kwa kuwekeza katika mbegu ng'ombe waliochaguliwa ,kwa maana hiyo mbegu hizo zinakwenda kuwapatia mitamba ngombe majike wanapokwenda kupandikiza wanakuwa na uhakika wa kupata majike ambayo yatakwenda kuwapatia kiasi kikubwa cha maziwa.
Joachim Balakana ni kiongozi wa mradi Jumuishi wa kuboresha maisha ya wafugaji wadogo kupitia maziwa ( DNA-BILD)unaofadhiliwa na serikali ya Sweeden kupitia kwenye ubalozi wao nchini Tanzania na umefadhiliwa kwa kiasi cha shilingi Bil.3 sawa na usd mil1.4 mradi huo umekuwa ukifanya kazi katika mkoa wa Kilimanjaro,Arusha na Tanga kwa upande wa wanufaika umefanya kazi katika mnyororo wa thamani wa maziwa,mzalishaji,muuza pembejeo msindikaji na kumfikia mlaji.
Mradi umeweza kufikia wafugaji 16,000 katika mikoa yote mitatu,vilevile wamepata elimu,ambayo imewawezesha kuongeza uzalishaji pamoja na utunzaji wa malisho mbegu za malisho miti malisho.wauz pembejeo wamepata ufadhili kupitia mfuko wa challenge fund aimewasaidia kupata mtaji kazi pamoja na vifaa vya juwasaidia uzalishaji wao, wasindikaji wamepata mitambo ya kuzalisha na kuongeza ufanisi katika uzalishaji maziwa na kufanya maziwa yao kuwa bora
Aidha amesema kuwa kwa watumiaji wameendesha kampeni kwa kipindi chote cha miaka 3 lengo lilikuwa kufikia watu 10,000 kwenye mradi huu tumeweza kuvuka lengo na tumeweza kufikia watu zaidi ya mil 2.3,kwa tathmini ambayo walikuwa wamejiwekea walilenga kufikia wafugaji 15,000 lakini wameweza kufikia wafugaji 16,000 tulitegemea kuwafikia wasindikaji 27wameweza kufanya kazi na wasindikaji 22ikiwa ni zaidi ya asilimia 80% wauza pembejeo lengo lilikuwa ni kuwafikia zadi ya 36 tumefanya kazi na 35 zaidi ya 90% kwa ujumla ukiangalia huo mradi ni mradi uliofanikiwa na kuvuka lengo
Jacquiline Peter Ngasa, ni Mkurugenzi mwendeshaji wa kampuni ya Asili Dairy Company Limited ameishukuru Taasisi hiyo kwa Mradi wa Dairy Nourish Africa BILD kwani abla ya mradi huo kuwafikia walikuwa wanapata changamoto ya vifaaa vya usindikaji wa bidhaa za maziwa ila kupitia DNA-BUILD wameweza kupata mafunzo ambayo yamewasaidia uzalishaji pamoja na kupunguza hasara ya kuharibu maziwa
Vilevile amesema kuwa wameweza kupata teknolojia ya kisasa kwaajili ya kuchakata maziwa hivyo tunawashukuru kwa sapoti yao na ameahidi kutumia vyema Naa FIFA na elimu waliyoipata kwaajili ya manufaa yao na jamii kwa ujumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...