Na WMJJWM- New York 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu .

Wakili Mpanju amesema hayo   Juni 12,  2025, katika Kikao cha 18 cha Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (CRPD) ya Umoja wa Mataifa (COSP18) kilichoanza  tarehe 10 Juni 2025 jijini New York nchini Marekani. 

Wakili Mpanju amesema Tanzania imechukua hatua ya kuunganisha watu wenye ulemavu katika mikakati ya kitaifa ya kupunguza umaskini ikiwemo unafuu wa kodi kwa vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu, kutoa mikopo nafuu kwa watu wenye ulemavu pamoja na asilimia 30 ya zabuni kwa makundi maalum wakiwemo watu wenye ulemavu.

"Tanzania chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepiga hatua kubwa  katika kutekeleza Mkataba huo na itaendelea kuweka Mikakati madhubuti ya utekelezaji wa Mkataba huo" amesisitiza Wakili Mpanju 

Ameongeza kwamba Tanzania imezindua Mkakati wa Taifa wa Teknolojia Saidizi  wa mwaka 2024 – 2027 ambao unatoa mwongozo wa kimkakati kwa sekta zote kuweka mazingira wezeshi ili kila mwenye uhitaji wa teknolojia saidizi aweze kupata kwa wakati na kwa gharama nafuu.

Wakili Mpanju ameongeza kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha haki za watu wenye ulemavu zinazingatiwa na kuwa msingi wa Usawa wa kijinisia nchini.

Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (CRPD) ya Umoja wa Mataifa (COSP18) unaangazia juhudi za kimataifa za kuhakikisha usawa na ujumuishaji kwa watu wenye ulemavu.





MWISHO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...