Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kanda ya ziwa limeteketeza Tani nne za bidhaa hafifu ikiwa ni pamoja na bidhaa za vipodozi, chakula, mifuko mbadala ( non woven) na nguo za ndani za mtumba zilizotumika zenye thaman ya Tsh. 12,712,000/=
Akizungumza na waandishi wa habari Juni 13.2025 katika dampo la Buhongwa lililopo jijini Mwanza, Afisa Udhibiti Ubora Shirika la Viwango Tanzania Bw.Donald Mkonyi amesema bidhaa zote zilizoteketeza zilikamatwa katika kaguzi zilizofanywa na TBS katika masoko kwa kipindi cha mwezi January hadi mwezi Mei mwaka 2025 katika Mikoa yote iliyopo kanda ya ziwa, Mara, Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga na Bukoba.
Bw.Mkonyi amesema kama bidhaa zilizoteketezwa kama zingeendelea kutumika zingeli sababisha athari kubwa za kiafya na uchumi kwa watumiaji na Taifa kwa ujumla.
"Zoezi hili la uteketezaji wa bidhaa ambazo hazina ubora zina jumuisha bidhaa za vyakula ambazo zimeisha muda wake wa matumizi,bidhaa za vipodozi zenye viambatanishi sumu,bidhaa zilizo haririwa tarehe za mwisho wa matumizi pamoja na bidhaa ambazo hazijasajiliwa nchini.
Ameongeza kuwa TBS itaendelea na ukaguzi katika maeneo ya biashara lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa bidhaa zinazouzwa zinakidhi matakwa ya viwango huku akiwateka wafanyabiashara hao kuhakikisha wanakuwa na utamaduni wa kukagua bidhaa za vyakula na vipodozi ili kujilizisha ubora wake na kuacha mara moja kuuza bidhaa zilizoisha muda wa matumizi ili kuepuka hatua za kisheria zinazoweza kuchukuliwa juu yao kwa kuuza bidhaa hafifu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...