Songea, Ruvuma

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu hatari ya kuharibu au kushughulika na miundombinu ya umeme bila idhini, hii ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Usalama wa Miundombinu ya Umeme iliyoanza tarehe 15 Juni 2025.

Katika ziara ya utoaji elimu iliyofanyika katika Kata ya Litapwasi Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Afisa Usalama Mkuu Msaidizi kutoka TANESCO Makao Makuu Shami Yusuph Dunia, ameeleza kuwa usalama wa miundombinu ya umeme ni jukumu la kila mwananchi, akisisitiza kuwa umeme hauna urafiki na unahitaji tahadhari kubwa.

Wananchi wanatakiwa kuwa walinzi wa kwanza wa miundombinu hiyo kwa kutoa taarifa pale wanapohisi uwepo wa watu wasioeleweka karibu na maeneo ya TANESCO.

TANESCO pia imeonya kuhusu uwepo wa watu wanaojifanya watumishi wa shirika hilo ili kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, imetolewa tahadhari kwa wananchi kutotoa fedha kwa mtu yeyote asiye na utambulisho rasmi, kwani shirika hilo hufanya kazi kwa kufuata taratibu za kiofisi pekee.

Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Ruvuma Alan Njiro, amehimiza wananchi kuchukua tahadhari wakati wa kuchoma mashamba kwa kuhakikisha nguzo za umeme zinalindwa dhidi ya moto, aidha ametoa wito wa tahadhari kwa kuona mtu yeyote karibu na transfoma au miundombinu ya umeme bila kuwa na vitambulisho rasmi vya TANESCO.

Amesema zaidi ya matukio 50 ya wizi wa nyaya za kopa yameripotiwa, na hivyo kuna haja kubwa ya ushirikiano kati ya wananchi na TANESCO katika kukomesha vitendo hivyo, mafundi halali wa TANESCO wana taratibu za kujitambulisha kwa viongozi wa maeneo husika kabla ya kuanza kazi, hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini na watu wasiowafahamu.

Diwani wa Kata ya Litapwasi Rajab Hassan Mtiula, amepongeza ujio wa TANESCO na kuahidi kuendeleza ushirikiano kwa kutoa elimu kupitia mikutano ya hadhara, amewataka wananchi kuacha mara moja tabia ya kuchoma mashamba karibu na nguzo za umeme, kwani kitendo hicho kinaweza kusababisha madhara makubwa kwa miundombinu.

TANESCO imeweka wazi kuwa kampeni ya utoaji elimu itaendelea nchi nzima kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja kuhusu umuhimu wa kulinda miundombinu ya umeme kama sehemu ya mchango katika maendeleo ya kijamii.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...