Na Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeingia Makubaliano na TanChin International kwa ajili wanafunzi wa VETA kupata ujuzi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa kutumia chuma.
Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA. Anthony Kasore amesema kuwa katika ushirikiano huo wanafunzi wanaosoma VETA watapata mafunzo ya ujenzi wa nyumba hizo pamoja kuwa sehemu ya miradi ya Tanchin katika kujifunza kwa vitendo.
Amesema kuwa moja ya nyumba ya mfano ya Tanchin itajengwa chuo cha VETA Kigamboni na wananchi wa eneo hilo watajifunza kupitia mradi huo.
Amesema kuwa VETA itatoa ushirikiano wa kutosha kwa TanChin katika kufanikisha makubaliano hayo kuwa matokeo chanya.
Aidha amesema ujenzi wa nyumba

hivyo ni fursa kwa VETA kupata kozi zinazoendana na mabadiliko ya teknolojia.
Amesema kuwa TanChin itatoa wataalam wa kufundisha wanafunzi wa VETA na baada hapo kupata mafunzo ya vitendo na baadae kuwa fursa ya ajira kwao.
Mkurugenzi wa TanChin Mansoor Khalfan amesema kuwa wanashukuru kuwa na makubaliano na VETA kutokana VETA inq vyuo nchi nzima na ni rahisi kuwafikia vijana wengi.
Amesema kuwa katika mafunzo hayo wanafunzi wa VETA watapata ujuzi wa ujenzi huo wa nyumba za chuma na kuwa na mchango katika sekta ya ujenzi wa nyumba nchini.
Kwa upande Mkurugenzi wa TanChin Paul Hu amesema kazi yao kupeleka teknolojia hiyo kwa watanzania kupitia VETA.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore akisaini mkataba wa Makubaliano na Mkurugenzi wa TanChin International Mansoor Khalfan kwa ajili ya Wanafunzi wa VETA kufundishwa ujenzi wa nyumba kwa kutumia chuma,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore akizungumza mara baada ya kusaini mkataba wa Makubaliano na TanChin International kwa ajili ya Wanafunzi wa VETA kufundishwa ujenzi wa nyumba kwa kutumia chuma,jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...