Na Mwandishi wetu - Dodoma
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Dodoma Joseph amesema vikundi 467 vinatafutwa na halmashauri hiyo kwa ajili ya kurejesha mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Serikali kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu hapa Nchini.
Fungo ameyabainisha hayo leo jijini Dodoma katika semina ya mafunzo yaliyoandaliwa.na Benki ya CRDB kwa vikundi vilivyokidhi kupata mikopo ya asilimia 10,toka isimamishwe na Serikali kutolewa na halimashauri, badala yake itatolewa na Benki zilizoidhinishwa.
Fungo amesema fedha hizo ni deni ambalo liko mikoni mwa vikundi ambavyo vimekopeshwa na kukimbia na mikopo bila kuirejesha kwa wakati ili watu wengine nao wakopeshwe kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao.
"Deni la shilingi bilioni 1.2 liko mikononi mwa vikundi ambavyo vimekopeshwa bado tunaendelea kuwatafuta ili wazirejeshe na wengine wapate mikopo,"alisema Fungo.
Aidha amesema hivi sasa Halmashauri hiyo imetenga shilingi bilioni saba kwa ajili ya kuvikopesha vikundi ambavyo vitakidhi vigezo kutokana na kutembelewa na Benki ya CRDB ambayo imo kwenye orodha ya utoaji mikopo hiyo kwa makundi hayo.
Aidha mpaka sasa vikundi 12 kati ya 126 vilivyokabidhiwa kwa CRDB vilivyofuzu kupewa mikopo ni vikundi 12 huku vingine vikikutwa na kasoro ndogo ndogo ambazo benki hiyo kupitia wataalam wake wa utoaji elimu kuhusu matumizi ya fedha lakini pia kuwakagua biashara wanazofanya kama inakidhi mikopo walioomba.
"Naomba nyie mliokidhi vigezo vya kupata mikopo mkairejeshe kwa wakati tunahitaji kuona mtiririko wa urudishaji unakuwa bora kulingana na masharti ya uchukuaji kuboreshwa,"alisema Fungo.
Naye Bahati Atanasio mwanakikundi cha vijana kutoka Kata ya Chihanga ameiomba serikali kupitia halmashauri kutoa mikopo sahihi ilioombwa na vikundi ili mikopo hiyo iweze kukidhi mahitaji yao ya biashara walioiombea.
Atanasio amesema chanzo kikubwa cha vikundi kukimbia na mikopo ni kutokana na vikundi kupata mikopo midogo tofauti na ile ambayo wameomba kitendo ambacho kinapelekea wanakikundi kugombana na kila mmoja kutoweka.na kuacha kurejesha mikopo.
Kutokana na hilo,ameiomba Serikali kupitia halmashauri zake kutoa mikopo kiasi kamili ambacho kikundi kimeomba ili waweze kutimiza malengo ya kikundi kitendo ambacho kitaepusha watu kukimbia na mikopo.
Naye Mkuu wa Kitengo wa Idara ya biashara ya biashara cha CRDB Benki Foundation Fadhili Bushagoma amesema wametembelea vikundi vote 126 kwa kushirikiana na ofisi ya halmashauri ya jiji la Dodoma,lakini vilivyo kidhi vigezo mpaka sasa ni vikundi 12 ambavyo viko tayari kupewa mikopo.
Bushagoma amesema vikundi vingine vimekutwa na changamoto mbalimbali ikiweno biashara waliotaja ni ndogo kuliko mkopo walioomba na kuongeza kuwa ambao hawajakidhi vigezo bado wana nafasi ya kujirekebisha ili wapate mikopo hiyo.
Mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri mbalimbali ilisitishwa kutolewa na Serikali ambapo hivi sasa imeaanza kutolewa na benki zilizoidhinishwa lengo ikiwa ni kupata walengwa wenye vigezo kutoka kwa wataalam wa fedha wa Benki.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...