Kampuni ya Vodacom Tanzania ikishirikana na Benki ya Stanbic imezindua jezi ambayo itatumika kwenye msafara wa Twende Butiama ya 2025

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire, amesema kuwa wameungana na Benki hiyo ili kuweza kufanikisha kampeni hiyo ya Twende Butiama ambayo ni ziara ya waendesha baiskeli Nchini,inayolenga kuchochea maendeleo ya kijamii Katika sekta za Elimu, Afya na Mazingira.

"Katika kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa vitendo ndio maana sisi Vodacom Tanzania tunaungana na kushirikiana na jamii katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo Afya, Elimu na utunzaji wa Mazingira"amesema Besiimire.

Akizungumza mwakilishi kutoka Stanbic Banki Wilmot Ishengoma kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Stanbic Benki,Manzi Rwegasira amesema kuwa na wao wameungana katika ziara hiyo kwa kuchangia milioni Mia Moja kila mwaka ili kufanikisha zoezi hilo.

"Tanzania ni nyumbani maendeleo na ukuwaji wake ni juu yetu katika kupinga maadui watatu ambao ni ujinga umaskini na maradhi hivyo basi kwa kuzingatia hilo tukaguswa na huu msafara tuliona mwaka Jana mafanikio makubwa ambayo yalipatikana kwa jamii tukahamasika kuendelea hivyo basi mwaka huu tupo na mwakani na mwaka unaofuata na tutachangia shilingi milioni mia Moja kwa kila mwaka katika kuendesha shughuli hiyo, amesema.

Kauli mbiu ya msafara wa Twende Butiama 2025 ni Kupambana na maadui watatu wa maendeleo ambao ni Ujinga, umaskini na Maradhi.ambapo kwa mwaka huu washiriki kutoka Nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, Uganda,Rwanda,Burundi, Congo, Zambia,Malawi, Nigeria pamoja na Marekani watakuwepo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...