Na John Mapepele -OR TAMISEMI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi nchini kuwaachia watoto wa kike kusoma shule maalum za msingi na sekondari ambazo zimejengwa na Serikali.

Mhe. Rais ametoa kauli hiyo leo, Juni 16, 2025 Mkoani Simiyu alipozindua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Simiyu iliyogharimu takribani bilioni 4.5 ambapo amesema Serikali imejenga shule za aina kila mkoa ili kuwasaidia watoto wa kike.
Amesema Serikali imeamua kujenga shule hizo maalum za sayansi kwa watoto wa kike kwa kuwa walikuwa nyuma katika mkondo wa sayansi.

" Shule hizi zimekuja kama maalum kwa watoto wetu wa kike ili waweze kupata fursa ya kusoma masomo ya Sayansi na kuendelea na masomo ya juu". Amefafanua Mhe. Samia

Mhe Rais amesema katika kuboresha elimu nchini imejenga miundombinu muhimu kama mabweni, madarasa, maabala, nyumba za walimu, viwanja vya michezo na majiko ya kisasa yasiyotumia kuni.


Aidha, amesema pia Serikali inajenga shule maalum kwa watoto wa kiume katika mikoa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Simiyu ambapo amesisitiza kuwa watoto wengine ambao hawatapata fursa ya kuendelea na elimu ya juu wataweza kujiunga na VETA.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amemshukuru Mhe Rais kwa maono yake ya uwekezaji mkubwa katika elimu, afya, miundombinu, na utawala bora hapa nchini.

Mhe. Mchengerwa pia amemshukuru Mhe Rais kwa kuzindua Ofisi ya kisasa ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi hii leo kabla ya kuzindua shule hiyo.



Amesema zaidi ya bilioni 90 zimetumika kwa ajili ya kujenga Ofisi za Wakuu wa Mikoa 26 hapa nchini.

Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Simiyu kwa ziara ya kikazi mbali na kuzindua miradi chini ya Wizara ya TAMISEMI pia amezindua miradi kadhaa ya maendeleo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...