Na said Mwishehe, Michuzi TV
MWENYEKITI wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Utekelezaji wa Programu ya Kizazi Chenye Usawa Angellah Kairuki amesema Tanzania imefanya hatua kubwa katika juhudi zake za usawa wa kijinsia tangu walipokuwa viongozi wa kimataifa katika Mkataba wa Kizazi Chenye Usawa Mwaka 2021.
Pia amesema Tanzania imepunguza pengo katika ushirikishwaji wa kifedha,kupanua haki za ardhi kwa wanawake, kuanzisha marekebisho ya bajeti zinazozingatia jinsia, na kuunda zaidi ya masoko 3,000 ya uwezeshaji wa pili kiuchumi kwa wanawake.
Ametoa kauli hiyo leo Juni 3,2025 jijini Dar es Salaam wakati kikao kilichoandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum kilichokuwa na lengo la kujenga uelewa kuhusu programu ya kizazi chenye usawa kwa Wahariri wa vyombo vya habari
“Hizi ni hatua muhimu, lakini tunajua kuwa maendeleo yasiyoonekana hayana nguvu. Bila ya vyombo vya habari, juhudi hizi zinaweza kupuuzwa au kukosewa.Ndio maana ninyi, wahariri wetu, mna jukumu muhimu.
“Hadithi mnazozisimulia kuhusu usawa wa kijinsia zinaweza kubadilisha mtazamo wa umma, kuathiri sera, kufungua fursa za ufadhili, na kubadilisha maisha.Hadithi ya Tanzania katika Kizazi Chenye Usawa haiwezi kusemwa bila majina yenu, matangazo yenu, na mitazamo yenu,”amesema Kairuki.
Ameongeza kuwa wakati wanapofanya kazi kuimarisha haki na fursa za wanawake na wasichana, ni muhimu kuelewa kwamba hawaachi nyuma wavulana.Usawa wa kweli lazima uwe na umoja.
Pia amesema wanapaswa pia kusimulia hadithi za wavulana wanaokabiliana na mabadiliko ya majukumu ya kijinsia, wanaume wanaoshikilia usawa katika ofisi na vijiji, na jamii zinazojifunza kuthamini huduma, huruma, na uongozi wa pamoja huku akifafanua hiyo si safari ya ushindani, bali ni safari ya pamoja.
“Kwa pamoja, tunaweza kujenga taswira nzuri ya Tanzania kama mfano wa nchi inayoongoza katika kufikia usawa wa kijinsia. Tunatarajia kuona mabadiliko makubwa katika ufuatiliaji wa habari kuhusu usawa wa kijinsia.”
Awali Naibu Katibu Mkuu Wizara Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum sehemu ya jinsia na wanawake Felister Mdemu amesisitiza kuwa kikao hicho ni muhimu katika kujenga uelewa kwa Wahaririwa Vyombo vya Habari kuhusu Programu ya Kitaifa ya Kizazi Chenye Usawa inayoratibiwa na Wizara hii ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Akifafanua kuhusu programu hiyo,amesema Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alishiriki Mkutano wa Jukwaa la Kizazi chenyeUsawa uliofanyika Jijini Paris – Ufaransa kuanzia Juni 30 Juni hadi Julai 2, 2022 ambapo kupitia kikao hicho Tanzania iliwasilisha ahadi za Nchi na aliahidi kuwa kinara katika kutekeleza eneonamba mbili linalohusu Haki na Usawa waKiuchumi kwa Wanawake.
“Katika kuhakikisha utekelezaji wa ahadi za nchi unafanyika, Wizara yenye dhamana na masuala ya jinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi kwa kushirikiana na Kamati ya Kitaifa ya Ushauri kuhusu Utekelezaji wa Ahadi za Nchi, inayoongozwa na Angellah Kairuki, imeandaa Programu inayoitwa Tanzania ya Kizazi Chenye Usawa (Tanzania Generation Equality Program).
“Utekelezaji wa Programu hii utahusisha Wadau wa Sekta za Umma, Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi na Jamii katika kipindi cha Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26),”amesema na kuongeza Serikali kupitia Wizara yenye dhamana imeendelea kushirikiana na Wizara za Kisekta, Taasisi za Umma, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika kutekeleza Programu hiyo.
Amesema kuwa programu hiyo itatekelezwa kupitia maeneo manne ambayo ni Uwekezaji wenye mrengo wa kijinsia katika huduma na kazi za matunzo kwenye sekta ya umma na sekta binafsi, Kazi zenye staha kwa wanawake katika sekta rasmi na sekta isiyo rasmi.
Pia upatikanaji na umiliki wa rasilimali za uzalishaji kwa wanawake na kubuni na kutekeleza mipango ya uchumi mkuu inayozingatia jinsia, maboresho ya bajeti na motisha ili kupunguza idadi ya wanawake na wasichana wanaoishi katika umasikini.
Wakati huo huo akizungumza kwa niaba ya UN Women Mwakilishi Mkazi nchini Tanzania, Katherine Gifford, amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopiga hatua kubwa katika kutekeleza ajenda ya usawa wa kijinsia kupitia Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, ametumia kikao hicho kuhimiza umuhimu wa kujenga matumaini kwa Watanzania kupitia habari zenye kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika shughuli za kiuchumi, akisema,
Pia amesema ni Matarajio yake Wahariri wakishafahamu programu hiyo basi lile kusudio la kuwa na kizazi chenye usawa litatimizwa.”amesema Balile huku akitoa rai kwa wanawake kutokuwa na woga katika kuzungumza na vyombo vya habari katika kuelezea masuala mbalimbali katika jamii yakiwemo ya kijinsia.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...