Na Mwandishi Wetu

WANAFUNZI na wakufunzi wa vyuo TEHAMAvikuu kutoka Tanzania wameibuka washindi katika shindano la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) la Huawei lililofanyika jijini Shenzhen China, likishirikisha washindani 210,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Wanafunzi hao ni kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) walipata tuzo ya juu na tuzo ya mshindi wa pili. Shindano hilo lilihusisha mafunzo kwa vitendo, ubunifu na programu.

Wanafunzi waliopata tuzo ya juu ni Vida Mapunda (DIT), Joseph Msuya (UDSM), na Sigfrid Michael (UDOM). Katika nafasi ya pili, ikichukuliwa na Paul Nkingwa, Godlove Hipolite na Felix Kuluchumila wote kutoka UDOM.

Shindano hilo pia liliwatambua wakufunzi bora, ambapo Jumanne Ally kutoka (DIT) alipokea zawadi kuu na Dk. Alex Mongi kutoka (UDOM) akishika nafasi ya pili katika kitengo cha mfukunzi bora .

Shindano hilo linafanyika kila mwaka likilenga kuwapa wanafunzi ujuzi wa kufanya kazi katika mifumo ya kompyuta ikihusisha eneo la data na akili mnemba.

Pia linalenga kutoa matokeo ya kiubunifu ili kutatua changamoto za ulimwengu hasa katika sekta kama vile kilimo, huduma za afya na elimu.

Akizungumza katika shindano hilo, Mkurugenzi wa Mkakati wa Tehama ICT na Maendeleo ya Biashara wa Huawei, Ritchie Peng alisema shindano hilo linaunga mkono maono mapana ya kampuni hiyo ya kuwa na dunia inayotumia akili mnemba ifikapo mwaka 2030, kwa kuhamasisha ujumuishwaji wa kidijitali katika kufkia maendeleo endelevu ya dunia

Akizungumza baada ya kupata tuzo hiyo, mwanafunzi Vida Mapunda kutoka DIT alisema ushindi huo inawapa motisha ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kudhihirisha kuwa vipaji vya Watanzania vinaweza kushindana kimataifa.

Mkuu wa Chuo cha Teknolojia kutoka ndaki ya Habari na Mawasiliano (CoICT) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Baraka J. Maiseli- akipongeza uwekezaji wa serikali katika miundombinu ya TEHAMA.

Mkuu wa UDOM, Dk.Florence Rashidi alipongeza jitihada zinazofanywa na Huawei katika kusaidia sekta ya elimu kwa kuwawezesha wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya Tanzania kushiriki katika mafunzo ya vitendo na mashindano ya kimataifa.

Huu ni mwaka wa pili kwa wanafunzi kutoka Tanzania kufanya vizuri katika shindano hilo la TEHAMA, mwaka 2023-2024, wanafunzi watatu walitambuliwa kwa ufaulu mzuri.

Washiriki katika shindano hilo walitoka katika nchi 12 ambazo ni China, Brazil, Algeria, Morocco, Nigeria, Ufilipino, Singapore, na Serbia.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...