Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Mwanza

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Stephen Wasira amewasili mkoani Mwanza na kisha ataelekea mkoani Geita kwa ajili ya kuanza ziara ya siku tatu katika mkoa huo.

Wasira amewasili leo Juni 15 mwaka 2025 katika Uwanja wa Ndege Mwanza ambapo amepokelewa na viongozi wa Mkoa huo kisha amepata nafasi ya kumsalimia na kufamfariji Mama Getrude Mongella ambaye hivi karibuni ameondokewa na mumewe mzee Silvin Ibengwe Mongella aliyezikwa Mwanza.

Hata hivyo kesho Juni 16 mwaka huu Wasira ataanza ziara ya siku tatu katika Mkoa wa Geita ambapo atakutana na wana CCM na pia kushiriki vikao vya ndani ya Chama ngazi ya Wilaya na Mkoa vitakavyohusisha pia viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama na Serikali.

Mbali ya kuwa na ziara katika Mkoa wa Geita ,Makamu Mwenyekiti Wasira pia anatarajiwa kushiriki katika uzinduzi wa daraja jipya la Kigongo-Busisi mkoani Mwanza ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

Pia uzinduzi wa daraja hilo ambalo limejengwa katika Ziwa Victoria unatarajiwa  na kushuhudiwa pia na viongozi mbalimbali pamoja na maelfu ya wananchi wa Mwanza na mikoa jirani.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...