MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema kinachoitafuna CHADEMA kwa sasa ni matokeo ya misuguano iliyotokana na uchaguzi wa kupata viongozi wa juu wa chama hicho uliogubikwa na lugha za matusi na kukashfiana.
Ameeleza hayo alipokuwa akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha viongozi wa CCM Wilaya ya Nyasa, katika mji wa Mbamba Bay mkoani Ruvuma ambako anaendelea na ziara ya kuimarisha Chama.
Wasira alisema tangu CHADEMA walipomaliza uchaguzi wa kumpata mwenyekiti wao wamekuwa na misuguano.
“Baada ya ule uchaguzi wao kila mtu amechukua chake na mtu anaitwa Lissu naye akachukua virago vyake na sasa hawako pamoja ndio wakasababisha kupatikana CHAUMA.
“Afrika hakuna anayekufa bila mchawi, mchawi wa CHADEMA ni CHADEMA wenyewe kwa kuwa hawasikilizani na wanachama wao wanawaambia tukagombee ubunge wanaambiwa mna uchu wa madaraka tena wanaosema hivyo ni vijana wadogo.
“Godbless Lema amekuwa mbunge kwa miaka 10, Tundu Lissu amekuwa mbunge miaka 10, John Heche miaka mitano. Hivyo wamekuwepo bungeni, Mnyika amekaa bungeni miaka 10. Vijana wenzao wanataka kujaribu kugombea wanasema wana uchu wa madaraka, wale watu wabinafsi,” alisema.
Alisisitiza kuwa, hao ndio wamefanya chama hicho kisambaratike, hivyo aliwashauri watafute mganga wa kuwaagua.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...