Na Mwandishi wetu, Dodoma

Akifungua mafunzo ya siku moja tarehe 18 Juni, 2025 kwa wazabuni wa Mkoa wa Dodoma na mikoa Jirani, Jijini Dodoma, Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando amewaasa kujifunza matumizi ya moduli hiyo ili waweze kuitumia wakati wa kuwasilisha malalamiko na rufaa zitokanazo na michakato ya zabuni.
Bw. Sando amesema kuwa moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST inafaida kwa wazabuni, taasisi nunuzi na PPAA ikiwemo kuokoa muda, gharama na kuongeza uwazi na uwajibikaji. “Moduli hii ina okoa muda na gharama kwa mzabuni kwa kuwa hatalazimika kusafiri ili aweze kuwasilisha malalamiko au rufaa yake PPAA,” alisema Bw. Sando
Pamoja na mambo mengine, Bw. Sando amesema PPAA imeweza kushughulikia mashauri 177 yaliyotokana na michakato mbalimbali ya Ununuzi wa Umma, ambapo katika mashauri hayo, PPAA ilizuia utoaji tuzo kwa zabuni 37 kwa wazabuni wasio na uwezo wa kifedha pamoja na wale waliokosa sifa za kitaalamu za kutekeleza zabuni husika, kwa kufanya hivyo PPAA iliisadia Serikali kupata thamani halisi ya fedha katika miradi hiyo.
Kwa upande wa wazabuni walioshiriki mafunzo hayo wakiongozwa na Mhandisi Beda Labule, amesema kuwa utaratibu wa kuwasilisha rufaa kieletroniki umerahisisha zoezi la kuwasilisha malalamiko na kukata rufaa kwa wazabuni ambao hawataridhika na sababu za kuondolewa kwao ikilinganishwa na ilivyokuwa awali.
“Kama mtakumbuka awali mzabuni mwenye malalamiko au rufaa alipaswa kusafiri kwenda katika Ofisi za PPAA kuwasilisha rufaa yake, ila sasa baada ya Serikali kuweka Moduli hii ya kupokea na kushughulikia malalamiko imeturahisisha zoezi la kuwasilisha malalamiko yetu PPAA,” amesema Mhandisi Labule
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Jofenai Investment, Bi. Jofenai-joy Felician amesema moduli imerahisisha zoezi la uwasilishaji wa malalamiko yatokanayo na michakato ya ununuzi wa umma pamoja na kusaidia kuokoa gharama na muda pamoja na kuongeza uwazi.
“Mimi kama mzabuni nimewahi kupatwa na changamoto mbalimbali wakati wa uwasilishaji wa rufaa kwa wakati, ni imani yangu kupitia moduli hii itasaidia pia utunzaji wa kumbukumbu za taarifa za rufaa ambazo zitakuwa zinawasilishwa katika michakato yote ya ununuzi wa umma,” amesema Bi. Felician
Mafunzo hayo ya siku moja kwa wazabuni wa Mkoa wa Dodoma na mikoa Jirani yanafuatia mafunzo ya awamu ya kwanza yaliyofanyika Kanda ya Ziwa tarehe 4 – 6 Februari, 2025 yalijumuisha mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Kagera, Simiyu na Shinyanga.
Aidha, awamu ya pili ya mafunzo yalifanyika Kanda ya Kaskazini tarehe 10 Aprili, 2025 yakijumuisha mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Kadhalika, mafunzo ya awamu ya Tatu yalifanyika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini tarehe 29 na 30, 2025 ambapo yalijumuisha mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Rukwa.
Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando akifungua mafunzo ya siku moja kwa wazabuni wa mkoa wa Dodoma na mikoa Jirani (hawapo pichani) jijini Dodoma.

Sehemu ya wazabuni/washiriki wa mafunzo ya Moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST kutoka mkoa wa Dodoma na mikoa Jirani jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando akifungua mafunzo ya siku moja kwa wazabuni wa mkoa wa Dodoma na mikoa Jirani jijini Dodoma
Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando aliyekaa katikati kwenye picha ya pamoja na Meneja wa Huduma za Taasisi, Bw. Paschal Kajuna (aliyekaa kushoto), Mkuu wa Sehemu ya Huduma za Sheria Bi. Agnes Sayi (aliyekaa kushoto) katika picha ya pamoja na watoa mada Jirani jijini Dodoma.
Meza Kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wazabuni wenye mahitaji maalum walioshiriki mafunzo ya Moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST kutoka mkoa wa Dodoma na mikoa Jirani jijini Dodoma.
Meza Kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST kutoka mkoa wa Dodoma na mikoa Jirani jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...