Serengeti-Mara.
POLISI Kata wa Kata ya Ikoma Wilaya ya Serengeti mkoani Mara Sajenti Emmanuel, ametoa wito kwa wazazi kutokuwa chanzo cha mmomonyoko wa maadili kwa watoto wao.

Ametoa kauli hiyo wakati akitoa elimu ya Polisi Jamii kwa wananchi wa kitongoji cha Momorogoro kijiji cha Robanda, kata ya Ikoma, katika mwendelezo wa kampeni ya Elimu ya Nyumba kwa Nyumba.

Katika maelezo yake, Sajenti Emmanuel amewakumbusha wazazi kuwa wanalo jukumu kubwa la kuiandaa vyema kesho ya watoto wao kwa kuwapatia malezi bora, ambayo yatawasaidia kuwa watu wenye tija na mafanikio katika nyanja za elimu, afya, na uchumi.

Aidha, aliwasisitiza wazazi kuwafundisha watoto wao kuvaa mavazi ya heshima yanayomstiri mtu, kudumisha usafi wa mwili, mavazi, na mazingira yanayowazunguka, kama njia ya kulinda maadili yao.

Aliwakumbusha wazazi kuwa urithi wa kudumu ambao wanaweza kuwaachia watoto wao ni elimu, alisema itawapatia maarifa muhimu katika kipindi chote cha ukuaji wao na kuwasaidia kuwa watu wanaofaa na kuheshimika katika jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...