Na Pamela Mollel,Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Paul Makonda amewataka madiwani wote kwenda kuwa mabalozi wazuri wa kazi zilizofanywa na serikali ya Rais Dkt,Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mwana mageuzi wa kiuchumi nchini Tanzania

Ametoa Rai hiyo leo juni 20,2025 wakati akiongea katika baraza la madiwani jiji la Arusha ambapo mabaraza yote nchini yamevunjwa leo kwa mujibu wa sheria ili kupisha uchaguzi Mkuu

"Leo tunavunja baraza letu la madiwani,naomba mkawe mabalozi wazuri katika maeneo yenu,yapo mema ambayo Rais Samia kayafanya kwa Mkoa wa Arusha,hayo yote mkayaseme kwa wananchi "Anasema Makonda

Aidha amemuomba Mkurugenzi wa jiji hilo John Kayombo kuhakikisha madiwani hao wanapata stahiki zao kwa wakati ili waweze kutumia katika shughuli zao binafsi ikiwemo za kisiasa

"Mkurugenzi naomba madiwani wapate stability zao kwa wakati lakini pia wenyeviti wote wa serikali za mitaa na kitongoji wanapata malipo yao kwa wakati "Anasisitiza Makonda

Wakati huo huo Waziri wa TAMISEMI,Mohamed Mchengerwa amevunja mabaraza yote nchini huku akiwataka madiwani wote waliopatia vitendea kazi ikiwemo Vishkwambi kutorudisha badala yake wabaki navyo kwa kuwa humo ndani wameweka mambo yao ya siri

Alitoa kauli hiyo leo wakati akizungumza kwa njia ya simu ya mkononi kwa baraza la madiwani jiji la Arusha kupitia simu ya Mh, Makonda baada ya kumuunganisha ili aweze kuongea na madiwani hao

"Namshkuru sana Mh.Makonda kwa kuniunganusha nanyi ili niweze kutoa kauli kwa mabaraza yote nchini ambayo yamekoma leo"Anasema Mchengerwa

Pia aliwapongeza Mameya Manaibu Meya,Wenyeviti wa Halmashauri za miji na Wilaya kwa kazi zao huku akiweka wazi kuwa kazi zao zimeandikwa katika kitabu cha dhahabu kwasababu wametumikia Nchi pamoja na Wananchi




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...