Ukipata muda naomba nipandishie hiyo nimefika kama rooving mdau akasema kwenu kuna mtu mmoja hua anakuja kuchukua story ni kibonge hivi nikamwambia huyo ni Ahmad akasema ndiyo huyo
Meneja wa Kituo cha Ukakiki wa Vipimo kilichopo Misugusugu Kibaha Mkoani Pwani Charles Mavunde akiwa ameshika mita ya TANESCO  ambazo ziko kwenye utaratibu wa kuhakikiwa.

Na Khadija Kalili, Michuzi TV
MENEJA wa Kituo cha Ukakiki wa Vipimo (WMA) kilichopo Misugusugu Kibaha Mkoani Pwani Charles Mavunde amesema Sheria ya Vipimo Sura 340

inataka vipimo vinavyotumika kupima ujazo, urefu na uzito wakati wa kupima bidhaa au kuhudumia Wananchi lazima vihakikiwe kila baada ya miezi 12 na Wakala wa Vipimo (WMA) nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kwenye mahojiano maalum Mavunde amesema kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo iliyoanza kufanya kazi mwaka 2002 baada ya kufanyiwa marekebisho Sura 340 kifungu namba 19 inataka vipimo vinavyotumika kupima katika biashara na huduma nyingine za kijamii lazima vihakikiwe kila baada ya miezi 12.

"Katika uhakiki huu Wakala Wa Vipimo nchini tunazingatia Sheria ya Vipimo iliyoanza kufanya kazi mwaka 2002 baada ya kufanyiwa marekebisho sura 340 kifungu namba 19 inataka vifaa vinavyotumika kupima lazima vihakikiwe kila baada ya miezi 12," amesema Mavunde.

Ameongeza kuwa sheria inatoa adhabu kwa mtu ambaye hata hakiki vifaa vinavyotumika katika kubebea au kupimia ambapo faini ni kati ya Sh. 100,000 hadi Mil.20 au kifungo jela miaka miwili.

"Kipimo chochote kinachopima mtaani katika kuhudumia Wananchi kinatakiwa kufanyiwa uhakiki kila baada ya miezi 12 lakini nawapongeza wananchi kwa kuwa na mwamko kwenye uhakiki wa dira za maji ni mkubwa" amesema Mavunde.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa pindi wanapopata changamoto za kuhisi ankara kubwa kutoka mamlaka husika hurnda dira hazipo sahihi ili kila mtu alipe na kufaidika kutoka kwa mtoa huduma na mpokeaji wa huduma.

"Uhakiki huo bado unaendelea hivyo Wananchi washirikiane WMA na sisi tupo tayari kuwahudumia kikubwa watoe taarifa mapema kwa mamlaka husika,"amesema Mavunde.

Amebainisha kuwa faida za kuhakiki mita za umeme na maji husaidia mwananchi kulipa fedha kihalali na mamlaka hupata makusanyo sahihi na yenye faida yaliyolipwa na mteja.

"Tuna hakiki vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na mita za maji, mita za umeme, malori ya mafuta na hata yale yanayosafirisha vimiminika ikiwemo gesi na kitu chochote ambacho kinatumia vipimo,"amesema Mavunde.

"Uhakiki wa vipimo una manufaa makubwa kwani ndiyo unaoweka pande zote kupata haki sawa kwa upande wa mteja na mtoa huduma au mfanyabiashara,"amesema Mavunde.

Mavunde ametoa wito kwa mamlaka mbalimbali na wananchi kushirikiana na (WMA) ili kuboresha suala la uhakiki wa vipimo ili kusitokee upande mmoja ukaumia na suala la uhakiki linasaidia serikali kuongeza mapato kwa usahihi wa vipimo mbalimbali.

Amesema wanatarajia kuhakiki mita za maji zaidi ya 87,000 kufikia mwishoni wa mwezi Juni 2025, ili kutambua usahihi wake kabla ya kwenda kufungwa kwa mteja.

Meneja Mavunde amesema kuwa kituo hicho kimefanya zoezi la uhakiki wa mita za umeme zaidi ya 5,500 za umeme mkubwa wa viwanda vya Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa mingine ili kuona kama zipo sahihi kulingana na matumizi viwandani.

Amesema kwa sasa wanaendelea na uhakiki huo sanjari na mita za umeme za majumbani na lengo la kufanya uhakiki huo ni kuzingatia usahihi wa vipimo kwa taasisi zinazosimamia ikiwemo TANESCO na mamlaka za maji na watumiaji wa mwisho ambao ni wateja.

Amefafanua kwa kusema kuwa uhakiki wa matanki yanayobeba vimiminika hufanyika na wanavipimo vyao maalumu vya kupima tanki ambavyo wanaviweka kwenye magari na hakuna udanganyifu ama ukwepaji wa aina yoyote unaoweza kufanyika"amesema Mavunde.

Hadi sasa tayari malori yabebayo vimiminika yapatayo 5, 900 yamepimwa katika kipindi cha Julai hadi Mei 2025 ambapo pia wamevuka lengo.

Kwa upande wa dira za maji katika kipindi cha Julai hadi Mei mwaka huu tayari gari 57,997 zimehakikiwa huku amesema kuwa wanao uwezo wa kuhakiki mita 100,000 kwa mwaka huu huku mita 30,000 za DAWASA zimeletwa ili zihakikiwe.

Amevitaja vituo vya WMA vya uhakiki wa malori yabebayo vimiminika vipo Mtwara, Mwanza na Iringa huku amesisitiza kwa kusema kuwa uhakiki huo hufanyika kwa malori ya ndani na nje ya nchi.

Naye Ofisa Vipimo Mkuu Gaudence Gaspery amesema kuwa hivi sasa wanahakiki mita za maji kwa kutumia mtambo wa kisasa.

Gaspery amesema kuwa mtambo huo wa kuhakiki una uwezo wa kuhakiki mita 10 kwa wakati mmoja na baada ya kuhakikiwa na kuonekana zinafaa kwa matumizi huwekewa rakili yenye rangi yanchungwa na ambazo zitagundulika zinahitaji kufanyiwa marekebisho hurekebishwa huku zile ambazo zitagundulika kwamba hazifai katika matumizi huteketezwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...