Katika maonesho ya Sabasaba mwaka huu, wadau wa elimu Beyond Schools wamewasisimua wengi kwa kuzindua mpango mpya wa kusoma elimu ya sekondari kwa njia ya mtandao, kwa kufuata mtaala rasmi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).

Akizungumza kwenye banda lao, Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Beyond Schools, Bi Gloria Mbbawile amesema mpango huo unalenga kusaidia wanafunzi walioko mbali na shule, waliokosa nafasi ya kujiunga na sekondari, au wenye changamoto za kiafya na kimazingira, kupata elimu bora popote walipo.

“Tunatoa fursa ya kujifunza masomo yote ya sekondari kupitia mfumo wa kidijitali, huku mwanafunzi akiwa na uwezo wa kuwasiliana na walimu ana kwa ana kwa njia ya mtandao au kwa ratiba maalum ya kukutana moja kwa moja,” amesema Bi Gloria.

Mpango huo unalenga kuondoa vikwazo vya kijiografia na kiuchumi kwenye upatikanaji wa elimu, huku ukiahidi kutoa ubora sawa na ule wa darasani. Beyond Schools imetoa mwito kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuutumia mfumo huo kama njia ya kuongeza fursa za elimu kwa vijana.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...